Mkurugezni mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Bi. Jane Mutagurwa akiwa amesimama mbele ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
DED Kiteto kuburutwa
mahakamani
Na Mohamed Shaabani Manyara
MKURUGENZI mtendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Kiteto Bi.
Janne Mutagurwa anakusudiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha
Diwani wa kata ya Sunya Mussa Briton kuwa amekula fedha za ujenzi wa Sekondari
Tsh laki sita na nusu.
Akizungumza hayo Diwani huyo baada ya kumalizika siku saba alizotoa
kwenye kikao cha baraza la madiwani kumtaka mkurugenzi huyo kuthibitisha madai hayo alisema,
kwa kuwa mkurugenzi ameshindwa kuthibitisha madai hayo yeye atamfikisha mahakamani
Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuchafuliwa kisiasa kwa
kutumiwa watendaji na nyaraka za Serikali kuwa amehujuma mradi wa ujenzi wa
sekondari ya Sunya iliyopo wilayani hapo na kuongeza kuwa hakuhusika kufuja
fedha hizo
“Kazi ya diwani ni kuhamasisha maendeleo ya kata yake ili
yaweze kusonga mbele, mimi sio mhasibu
wa kamati ya mradi wowote ndani ya kijiji au kata sasa inakuwaje nituhumiwe
kuhujumu mradi tena kwa kuandikwa kwenye makabrasha ya vikao vya Halmashauri”?
“Kamati ya fedha na mipango imepitisha na kubariki kuletwa
taarifa hii kwenye kikao cha madiwani, naamini walioyaleta hapa wana uhakika ya
walichokiandika na kwa bahati nzuri taarifa hii ni ya mkaguzi wa ndani wa
Halmashauri aliyotumwa na mkurugenzi ningependa sheria ifuate mkondo wake”Alisema
Bw. Briton
Hata hivyo Diwani Braitoni aliliambia gaeti hili kuwa tayari
amekwisha kuwasiliana na wakili wake ambaye kwa sasa wamepanga kuandika barua
maalumu (notes) ya siku ishirini na moja kwa mkurugenzi ya kuonyesha nia hiyo
ya kumshitaki kwa kushindwa kutimiza matakwa ya diwani huyo kusafishwa ndani ya
kata yake
Aidha hoja hiyo ilivuta hisia kwa wawakilishi hao wa wananchi
kwa kumtaka diwani huyo awe na subira na kuacha uamuzi wake huo wakisema kuwa
uchunguzi wa kina ufanyike zaidi kubaini ukweli ya suala hilo ambalo lina
taswira ya kuchafuliwa kisiasa
Akizungumza hayo Diwani Kone Lembile wa kata ya Kijungu
alisema hakuna haja ya Diwani huyo kuhamaki kwani kama jambo hilo sio kweli
haliwezi kuleta madhara kwake, lakini kama atakuwa amehusika hapo ndipo shida
inaweza kutokea
Akiendelea na hoja hiyo huku akikatishwa na diwani huyo
Lembile alisema, wananchi kwa nafasi zao nao hupima kinachozungumzwa na kumtaka
diwani huyo kupuuza kauli hiyo ambayo inaonekana kuwa huenda kweli imemchafua
kiasiasa
Hata hivyo hoja hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa
Halmashaur i ya wilaya Mainge Lemalali kwa kumwomba Diwani huyo kuacha uamuzi
huo akisema kuwa atahakikisha jengo hilo linakamilishwa na kuachana na mvutano huo
wa kisiasa
“Mhe. Briton tukiachana na suala la umri nakusihi achana na uamuzi
wako huo, kwani haya yataweza
kuchelewesha maendeleo ya wananchi wakati tunaweza kukaa chini sisi na kutafuta
ufumbuzi, ili mwisho wa siku tuone maendeleo ya wananchi yanasonga
mbele”alisema Lemalali
Kauli hiyo ilizidi kuchochea hasira kwa diwani huyo na kutoa
uamuzi wa mwisho kuwa mkurugenzi huyo apite katika vitongoji na vijiji katika
kata yake hiyo ya Sunya kuelezea kuwa diwani huyo hakufuja fedha jambo ambalo
mkurugenzi huyo hakulifanya
Hata hivyo gazeti hili lililazimika kuongea na mkurugenzi
kuhusiana na tuhuma hizo na kusema kuwa ameshangazwa na uamuzi wa Diwani huyo
wa kutaka kumfikisha mahakamani na kuongeza kuwa akiwa kama katibu wa madiwani
hao atahakikisha kuwa wanayamaliza
Kuhusu kupita kwenye kata yake kutangaza kuwa diwani huyo
hakuhusika na ufisadi mkurugenzi huyo alisema kuwa ni mapema na wala jambo hilo
sio kubwa kama linavyo tafsiriwa na baadhi ya watu hasa wakidhani kuwa suala la
kumfikisha mkurugenzi mahakamani ni rahisi
Mwisho
Marehemu Julius alifariki mjini kibaya wakati akikimbizwa hospitali muda mfupi baada ya kuanguka nyumbani kwake akienda chooni
Hata hivyo uchunguzi uliofanya na Blog hii umebaini kuwa awali alikuwa akithumiwa juu ya kazi aliyokuwa amekabidhiwa na wenzake ya kuchangisha fedha kwaajili ya kuwaondoa wakulima Emboley Mortangos (mbunga)
Wafugaji walichangia fedha nyingi ambazo haikufahamika kwa haraka ili kusaidia kazi ya kuwaondoa wakulima katika maeneo hayo waliojikita kwa shughuli za kilimo jambo ambalo lilipingwa vikali na wakulima
Hata hivyo hali bado tete kati ya wakulima na wafugaji ambapo kila mara mapigano huibuka na kuleta maafa kati ya pande hizo wakigombea ardhi
Mkuu wa Wlaya ya Kiteto Bi. Martha umbulla amethibitisha kuibuka migogoro hiyo ya mara kwa mara akisema kuwa ameomba msaada uongozi wa Mkoa ili uweze kuingilia kati sakata hilo>
Maoni
Chapisha Maoni