HISTORIA YA MKOA WA MANAYARA



Mkoa wa Manyara ulianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 367 lililotolewa tarehe 27 Julai, 2002 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali tarehe 2 Agosti, 2002 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha ambao kabla na wakati wa kipindi cha Uhuru ulijulikana kama Jimbo la Kaskazini (Northern Province). Mkoa wa Arusha ulianza kutumia rasmi jina hilo mwaka 1963.Miongoni mwa Wilaya zilizounda Mkoa huo ni Mbulu na Maasailand ambazo sehemu kubwa  iko katika Mkoa wa Manyara sasa. Wilaya hizo ziligawanywa kama ifuatavyo:- Wilaya ya Mbulu ilianzisha Wilaya ya Hanang mwaka 1969  na Hanang ikianzisha  Babati mwaka 1985, wakati Wilaya ya Maasailand iligawanywa kwenye Wilaya ya Kiteto mwaka 1974 ambayo pia iligawanywa na kuanzisha Wilaya ya Simanjiro mwaka 1993. Aidha, baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha, Wilaya za Mbulu, Hanang’, Babati, Kiteto na Simanjiro ziliuunda Mkoa wa Manyara.







MAENEO YA UTAWALA
Mkoa umegawanyika katika Wilaya tano za kiutawala za Babati, Hanang’, Kiteto, Mbulu na Simanjiro; zote zikiwa na Halmashauri za Wilaya na pia Halmashauri ya Mji wa Babati. Kuna  Majimbo ya Uchaguzi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa  sita; Tarafa 29, Kata 123, Vijiji 393, Vitongoji 1,540 na Mitaa 35. Makao Makuu ya Mkoa yako Mjini Babati.
IDADI YA WATU
Katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002 Mkoa ulikuwa na watu 1,040,461 na ongezeko la 3.8% kwa mwaka, mpaka mwaka 2011 Mkoa unakadiriwa kuwa na watu 1,441,771.
WAKAZI WA MKOA
         Makabila Makuu katika Mkoa

WAKAZI WA WILAYA
KUNDI KUU
KUNDI DOGO
BABATI
Wabantu
Wambungwe,Warangi,Wachagga, Wapare, Wangoni,WaAsi
Nilo Hamites
Wagorowa, Wa-Iraqw, Maasai, Barbaig
HANANG’
Wabantu
Wanyiramba, Warangi, Wanyaturu
Nilo Hamites
Wabarbaig, Wa-Iraqw.
MBULU
Nilo Hamites
Wa-Iragw, Wabarbaig, Wahadzabe.
KITETO
Wabantu
Wagogo, Warangi, Wanguu, Wakaguru, Wasambaa na Wanguu
Nilo Hamites
Wamaasai, Waburunge, Wa-Akea (Wandorobo)
SIMANJIRO
Wabantu
Wanguu, Wachagga, Wapare, Warangi
Nilo Hamites
Wamaasai na Wandorobo[ Wa-Akea ]

NB: Kwa sasa kuna makabila mengine madogo madogo. Aidha makabila ya Hadzabe na Akea yanahitaji uangalizi kwa vile huishi kwa kutegemea uwindaji, mizizi, matunda na kula asali.

MIPAKA YA MKOA                                            
Mkoa umepakana na Mikoa ya Arusha Upande wa Kaskazini, Kilimanjaro na Tanga Upande wa Mashariki, Dodoma Upande wa Kusini, Singida na Shinyanga upande wa Magharibi.

MGAWANYIKO WA ENEO LA MKOA KWA MATUMIZI MBALIMBALI
Mkoa una eneo la kilometa za mraba 50,921, zikiwemo kilometa za mraba 49,661 za nchi kavu na kilometa za mraba 1,260 zilizofunikwa na maji.  Eneo la nchi kavu la Mkoa limegawanyika kama ilivyooneshwa katika jedwali lifuatalo:
Maeneo ya Utawala na Idadi ya watu

Wilaya /Mji
Eneo Km2
Tar-afa
Kata
Vijiji

Vitongoji
Mitaa
Idadi ya
Watu, 2011
Uwiano wa Watu kwa eneo (Density)
Babati Mji
461
2
8
13
54
35
*423,380
69.8
Babati
5,608
4
21
95
273
0


Hanang’
3,814
5
25
65
286
0
285,316
74.8
Kiteto
16,645
7
19
58
210
0
206,715
12.4
Mbulu
4,452
5
32
110
475
0
330,784
74.3
Simanjiro
19,941
6
18
52
242
0
195,576
9.8
Jumla
50,921
29
123
393
1,540
35
1,441,771
28.3

* Idadi ya Watu inajumuisha Halmashauri ya Mji wa Babati na Wilaya ya Babati
  
HALI YA HEWA YA MKOA
Mkoa unapata wastani wa Mvua kati ya mm 450 na mm1200 kwa mwaka. Kuna misimu miwili ya mvua. Mvua za muda mfupi ambazo hunyesha kati ya Oktoba na Desemba katika baadhi ya maeneo ya Wilaya za Kiteto, Hanang’, Babati na Mbulu. Mvua za muda mrefu hunyesha kati ya mwezi Februari na Juni. Hali ya hewa ni nyuzi joto 130C wakati wa masika na nyuzi 330C wakati wa kiangazi kutegemeana na msimu na mwinuko wa ardhi. Mkoa upo katika mwinuko kati ya mita 1000 – 2000 juu ya usawa wa bahari

Maoni