Maambukizi
ya VVU Ukimwi Manyara yapungua
NA. MOHAMED HAMAD
Takwimu za maambukizi ya VVU Ukimwi Mkoani Manyara zimepungua
kutoka 2% mwaka 2003 / 2004 hadi 1.5% kwa mwaka 2011 / 2012 kutokana na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Serikali
Kushuka kwa kiwango hicho kumetokana na jitihada kubwa zilizofanya
na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali pamoja na Idara mbalimbali katika kutaka
kupungua kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kilichopo
Akizungumza na mamia ya wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani
ambayo Kimkoa yalifanyika kata ya Engusero alisema Serikali inatambua kazi
zinazofanywa na Mashirika
“Serikali Mkoani Manyara itaendelea kutambua kazi nzuri
zinazofanywa na Mashirika ya Umma ndani ya jamii ambazo zimekuwa msaada mkubwa
kwa wananchi katika kuharakisha maendeleo yao lakini pia tunaziunga mkono”alisema
Ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni pamoja
Africare,Aid Relife, Injenda Helth na mengine kama KINNAPA ambayo yanafanya
kazi karibu na wananchi katika mapambano dhidi ya maambikizi ya Ukimwi
Akisima risala ya Mkoa Bi. Anna Fisoo mjumbe wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara alisema mafanikio ya kupungua kwa kiwango cha maambukizi
ya Ukimwi yametokana na jitihada kubwa zilizofanywa na mashirika ya Umma na
Serikali
Alisema utafiti unaonyesha kuwa ukimwi na malaria kwa
mwaka 2011/2012 Mkoa wa Manyara una kiwango cha maambukizi ya 1.5% tofauti na
baadhi ya Mkoa mingine hapa nchini
Kwa upande wa baadhi ya watu waishio na VVU Ukimwi wakizungumza
na RAI walisema kasi ya maambukizi ya Ukimwi itazidi kupungua endapo walengwa
watashirikishwa pamoja na kujengewa uwezo Kiuchumi
“Sisi tunaoishi na VVU Ukimwi wakati mwingine lishe inasumbua
sana, unapotumia dawa halafu huna chakuweka mdomoni unalazimika kutumia njia mbadala kama wengine
hata kujiuza ili waweze kuishi bila kujali madhara yanayoweza
kujitokeza”alisema
Lakini pia kuna tatizo la kunyanyapaliwa ndani ya jamii
jambo ambalo mtu anaeishi na VVU Ukimwi anajikuta kama sio mwanadamu na kukata
tamaa ya kumeza hata dawa kisha kupoteza
maisha
Kwa mujibu wa Mratibu wa HBC wa shirika la Africare
alitaja baadhi ya jitihada zinazofanywa na shirika lake kuwa ni pamoja na kutoa
huduma kwa WAVIU watu waishio na VVU Ukimwi na Wasendeka watu wenye magonjwa
Sugu kama Kisukari,Moyo,na Kifua Kikuu TB
Shirika la Africare hadi kufikia 2013 wameweza kufikia
WAVIU 3579 ambao wamepatiwa huduma ya kinga, kuwezeshwa kiuchumi,pamoja na
masuala ya Lishe ambayo yatawasaidia
wanapotumia madawa ya kurefusha maisha
Hata hivyo imeelezwa kuwa baadhi ya changamoto
zinazowakabili mashirika hayo kuwa ni
pamoja na watu wanaoishi na VVU Ukimwi kuhama vituo vya dawa hivyo kusababisha
kutopatikana kwa kumbukumbu sahihi.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni