MAAMBUKIZI YA UKIMWI YAPUNGUA KITETO 2012


Maambukizi ya VVU Ukimwi Manyara yapungua

NA. MOHAMED HAMAD
Takwimu za maambukizi ya VVU Ukimwi Mkoani Manyara zimepungua kutoka 2% mwaka 2003 / 2004 hadi 1.5%  kwa mwaka 2011 / 2012 kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Serikali

Kushuka kwa kiwango hicho kumetokana na jitihada kubwa zilizofanya na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali pamoja na Idara mbalimbali katika kutaka kupungua kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kilichopo

Akizungumza na mamia ya wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo Kimkoa yalifanyika kata ya Engusero alisema Serikali inatambua kazi zinazofanywa na Mashirika

“Serikali Mkoani Manyara itaendelea kutambua kazi nzuri zinazofanywa na Mashirika ya Umma ndani ya jamii ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kuharakisha maendeleo yao lakini pia tunaziunga mkono”alisema

Ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni pamoja Africare,Aid Relife, Injenda Helth na mengine kama KINNAPA ambayo yanafanya kazi karibu na wananchi katika mapambano dhidi ya maambikizi ya Ukimwi

Akisima risala ya Mkoa Bi. Anna Fisoo mjumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara alisema mafanikio ya kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya Ukimwi yametokana na jitihada kubwa zilizofanywa na mashirika ya Umma na Serikali

Alisema utafiti unaonyesha kuwa ukimwi na malaria kwa mwaka 2011/2012 Mkoa wa Manyara una kiwango cha maambukizi ya 1.5% tofauti na baadhi ya Mkoa mingine hapa nchini

Kwa upande wa baadhi ya watu waishio na VVU Ukimwi wakizungumza na RAI walisema kasi ya maambukizi ya Ukimwi itazidi kupungua endapo walengwa watashirikishwa pamoja na kujengewa uwezo Kiuchumi

“Sisi tunaoishi na VVU Ukimwi wakati mwingine lishe inasumbua sana, unapotumia dawa halafu huna chakuweka mdomoni  unalazimika kutumia njia mbadala kama wengine hata kujiuza ili waweze kuishi bila kujali madhara yanayoweza kujitokeza”alisema



Lakini pia kuna tatizo la kunyanyapaliwa ndani ya jamii jambo ambalo mtu anaeishi na VVU Ukimwi anajikuta kama sio mwanadamu na kukata tamaa ya kumeza hata dawa  kisha kupoteza maisha

Kwa mujibu wa Mratibu wa HBC wa shirika la Africare alitaja baadhi ya jitihada zinazofanywa na shirika lake kuwa ni pamoja na kutoa huduma kwa WAVIU watu waishio na VVU Ukimwi na Wasendeka watu wenye magonjwa Sugu kama Kisukari,Moyo,na Kifua Kikuu TB

Shirika la Africare hadi kufikia 2013 wameweza kufikia WAVIU 3579 ambao wamepatiwa huduma ya kinga, kuwezeshwa kiuchumi,pamoja na masuala ya Lishe  ambayo yatawasaidia wanapotumia madawa ya kurefusha maisha

Hata hivyo imeelezwa kuwa baadhi ya changamoto zinazowakabili mashirika hayo  kuwa ni pamoja na watu wanaoishi na VVU Ukimwi kuhama vituo vya dawa hivyo kusababisha kutopatikana kwa kumbukumbu sahihi.

Mwisho

Maoni