Mauaji
yakutisha Kiteto
· -- Wakulima wavamiwa, wachinjwa
· -Risasi za moto zatumika
· -Wachomewa nyumba zao
· -RC Manyara awasili kuwapa pole
Na
Mohamed Hamad
WILAYA
ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama
baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi
Miongoni
mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa
Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake
usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa
kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada
ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao
mafuta aina ya petrol kisha kuwasha moto
Akizungumza
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho
alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na
vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani
“Nilichomewa
Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula,
lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio
nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema
chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye
shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga
kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo
Hata
hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika
Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni
uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana
Akielezea
hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya
Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi
kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja
Kwa
upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo
kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika
Hata
hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa
Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika
hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai
“Baada
ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo
la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto
ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga
mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji
Waliofariki
katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo,
Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo
pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa
kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga
Waliolazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21)
Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na
Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu
Hata
hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho
aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua
wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi
wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora
kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za
jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja”alisema Mbwillo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni