Wakulima,Wafugaji
wanusurika kuzichapa Kiteto.
·
Ni baada ya kutofautiana kauli kwenye mkutanoni
·
Polisi
waingia mitini,wadai walitumia busara
NA.MOHAMED
HAMAD MANYARA
Mkutano
maalumu uliokuwa umeitishwa na baadhi ya vijana wa jamii ya Kifugaji Wilayani Kiteto
kujadili mgogoro wa ardhi katika eneo la Emboley Murtangos umeingia dosari
mjini Kibaya baada ya pande hizo kutofautiana kauli
Awali
akizungumza kwenye mkutano huo mmoja wa wanajamii ya kifugaji Abel Mainge
alisema lengo la mkutano huo ni kuleta maridhiano kati ya wakulima na wafugaji
ambayo yalitoweka na kusababisha madhara mbalimbali yakiwemo maafa katika pande
hizo
Wakati pande
hizo zikitunishiana misuli Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto lilishindwa
kuingilia kati kutuliza mzuka wa wananchi uliodumu kwa zaidi ya saa moja na
nusu hadi walipoamua kuachana wenyewe kwa kuvunjika mkutano huo maalumu
“Leo ni siku ya
peke kufanya mkutano mkubwa bila kuwa na viongozi wetu, nia ni kutaka kuwekana
sawa ili tuweze kuishi kwa amani kwani kila mara tumekuwa tukishuhudia maafa
yanayotokana na kugombania ardhi”alisema Abel
Wakati hayo
yakisemwa msafara wa madereva wa pikipiki almaarufu Bodaboda waliingia na
ujumbe maalumu juu ya kilio chao cha kukataa kuondolewa watu walioitwa wavamizi
kutoka wilaya na mikoa mbalimbali hapa nchini katika eneo la Emboley Murtangos
Ghafla hali
ilibadilika badala ya madereva hao kuja na mabango ambayo hayakutarajiwa kwenye
mkutano huo ambao uliokuwa na waandishi wa magazeti na Televisheni wakipika
picha kwaajili ya kuripoti ktika vyombo vyao vya habaro juu ya matukio hilo
Baadhi ya
mabango hayo yalisomeka kuwalaumu viongozi wa Wilaya, Mkoa, na Taifa kwa
kushindwa kuingilia kati kutatua migogoro ya ardhi,Kutotambuliwa kwa eneo la
Emboley Murtangos, pamoja na kulaani ubaguzi wa Kikabila unaofanywa na baadhi
ya viongozi wa Wilaya ya Kiteto
Wakati hayo
yanajitokeza Polisi walifika kwenye mkutano huo wakiwa na kamera zao za video
na picha za mnato wakipiga picha malumbano kati ya pande hizo kabla ya kuanzwa
kwa mkutanona kisha kutoweka kusiko julikana hadi vurugu zilipoisha
Hata hivyo
RAI lililazimika kuzungumza na baadhi ya walinzi hao wa amani (Polisi) kuwa
kwanini waliondoka kwenye mkutano huo kwakuwa ulikuwa na kibali chao na kusema
hali haikuwa shwari na kwamba walilazimika kutumia busara kuondoka
“Mwandishi
wakati mwingine Polisi tunalazimika kutumia busara katika masuala kama haya,
tungeingilia kati tungezidisha mgogoro, tumelazimika kuondoka kidogo ili
waelewane wenyewe jambo ambalo pande hizo ziliachana kwa kuondoka kwenye
mkutano huo
Paulo Tunyoni
mtumishi wa shirika la MWEDO,Michael Williamu Afisa habari wa Halamshauri ya
Wilaya ya Kiteto,pamoja na Shukumu Tuke wa Shirika la CORDS na vijana wengine
wa waliokuwa wameandaa mkutano huo walisikika wakisema walikuwa na nia njema
kuunganisha wakulima na wafugaji badala yake imeshindikana
Kwa upande
wao wakulima wakiwakilishwa na Bakari maunganya alisema kamwe hawawezi kuridhia
kinachofanywa na wafugaji kwani wamekuwa wakiwasumbua kwa kuwafukuza katika
maeneo yao kwa kushirikiana na Serikali wakidai kuwa wameanzisha hifadhi ya
Msitu
Wakati hayo
yakijitokeza baadhi ya vijana wamesikika wakimlaumu Mbunge wa Jimbo lao la
Kiteto Benedict Ole Nangoro kuwa hawasaidii wanapopata matatizo kwa kuwa yuko
mbali nao kwa kuishi Dar es Salaam Kishuhuli
Mbunge wa
Jimbo la Kiteto ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amekuwa akifanya
shughuli zake Dar za Kiserikali na kwamba kukosemana kwake kumewafanya wananchi
wakose mtu wa kumweleza matatizo yao
RAI
limelazimika kuzungumza na na katibu wa Mbunge huyo Singo Ndoera na kusema
matatizo ya wanakiteto hayamalizwi na mbunge kuwepo Jimboni bali na kuongeza kazi
ya Mbunge sio kutatua migogoro ambayo ina vyombo vya utatuzi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni