MAUAJI YA KUTISHA KITETO

MAUAJI YA KUTISHA KITETO

Wakulima 2 wameuawa, 7 wajeruhiwa na wafugaji Kiteto • Mmoja achinjwa kama kuku • Wengine walazwa Hospitali ya Kiteto Na Mohamed Hamad Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wakulima wameuawa Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya kundi kubwa la wafugaji wamasai kuwavamia katika maeneo yao yaliyopo Kalikala na kuwakata kata mapanga huku mwingine akichinjwa kama kuku Waliouawa ni Juma Mlagwa 47 (mkulima) aliyechinjwa shingo,na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Yohana wakiwa kwenye makazi yao ambapo imedaiwa kuvamiwa la wafugaji wamasai na kusababisha vifo pamoja na majeruhi ya wakulima Kundi la wafugaji lililodaiwa kutenda tukio hilo lilitokea Kata ya Ndedo,Makami, na Njoro ambapo kwa pamoja waliungana wakiwa na silaha nzito za moto ,mapanga na fimbo kisha kuwavamia wakulima waliokuwa katika eneo hilo Awali akielezea sakata hilo mmoja wa majeruhi Habiba Ally (16) alisema chanzo cha tukio hilo ni wafugaji hao (wamasai) kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima aliyefahamika kwa jina la Msukuma ambaye aliwakataza bila mafanikio Ilielezwa mkulima huyo baada ya kushambuliwa akiwa na mke wake shambani walienda kutibiwa na kurejea nyumbani kwao, baada ya siku mbili liliibuka kundi kubwa la wafugaji na kuanza kuwashambulia wakulima katika maeneo hayo Kwa upande wake mwajuma hamisi (20) aliyepigwa risasi ya panjani akizungumza na RAI alisema akiwa nyumbani kwake usiku alisikia kelele na alipotoka nje alipigwa risasi kisha kuanguka chini ambapo hapo alifuatwa na kupigwa fimbo ya kichani na begani “Hawa wamasai walikuwa wanapiga risasi hovyo juu na hata pembeni na kila aliyetoka nje ya nyumba yake alikutana nao na kuanza kushambuliwa kwa mapanga na fimbo hali iliyosababisha wengi wetu kuletwa hapa Hospitali ya Kiteto”alisema Mwajuma Kwa mujibu wa daktari wa zamu ambaye hakutaka kutajwa majina yake alithibitisha kupokea maiti wawili pamoja na majeruhi saba akiwemo mwanamke mmoja aliyepigwa risasi na mwingine kijana wa miaka (16) ambaye hali yake ni mbaye amekatwa tumbo na utumbo wake kutoka nje Tukio hilo ni matokeo ya mkutano wa wafugaji ilioandaliwa na kuvurugika mjini kibaya kisha kundi hilo la wafugaji kuamua kuungana na wengine kutoka maeneo ya jirani kuvamia makazi ya wakulima waliopo eneo la Kalikala na kuwajeruhi Akizungumza na waandishi wa habari Paulo Tunyoni (mfugaji) hivi karibuni alisema wamechoshwa na wakulima waliovamia maeneo ya hifadhi na kuitaka Serikali iwaondoe la sivyo watachukua sheria mkononi kukabiliana na wakulima waliopo katika maeneo ya hifadhi Wakati kauli hizo zikitolewa na wafugaji Serikali Wilayani Kiteto imedaiwa kushirikiana na wafugaji kuwa wakulimawamevamiaeneo la murtangosi kuwa yalitengwa kama hifadhi ya msitu ambayo mahakama iliamuru pasifanyike shughuli za kibinadamu Bakari Maunganya mkulima Wilaya Kiteto alisema chanza cha migogoro hiyo ni viongozi kunufaika na upande mmoja wa wa wafugaji kwa kuwachangisha fedha na mifugo na kutumia kama vyanzo vya mapato yao Hata hivyo sakata la migogoro ya ardhi Wilayani Kiteto limezidi kuchukuwa sura mpya baada ya Job Ndugai Mb.Kongwa kusema katika moja ya vikao mji mdogo wa Kibaigwa kuwa kukithiri kwa mogogoro ya ardhi Wilayani Kiteto ni kuendeezwa kwa ukabila na Viongozi wa Wilaya Hali ya usalama eneo hilo bado tete na kwamba kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Akili Mpwapwa ametuma Kikosi maalumu cha Polisi kwaajili ya kulinda amani ambayo inahofiwa kuwa inaweza kuzidi kutoweka kwa kundi la wakulima kulipiza kisasi Naye mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bi Jane Mutagurwa alipopigiwa simu na RAI kuhusu tukio hili alisema kuwa hana habari na kuahidi kwenda kuona kilichotokea katika eneo hilo na hasa kuwaona majeruhi waliolazwa Mwisho

Maoni