Wanafunzi
32 walala chini kwa miaka mitano mfululizo
- · Ni kwa kukosa vitanda shuleni
Na. Mohamed Hamad KITETO
JUMLA ya wanafunzi wa kiume 32 wa shule ya msingi na
ufundi Kibaya iliyoanzishwa mwaka 1950 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara,
wanalazimika kulala chini kwa kukosa vitanda kwa zaidi ya miaka mitano
mfululizo
Wakizungumza hayo wanafunzi wanaoishi shuleni hapo wamesema kwa miaka mitano wamekuwa wakilala
chini kwa kukosekana vitanda baada ya vile vilivyokuwa vikitumika kuchakaa
Wamesema mbali na matatizo hao yanayowakumba pia shule
hiyo ina upungufu mkubwa wa samani na thamani hali inayosababisha usumbufu
mkubwa wanapokuwa shuleni
Wamesema shule ina upungufu wa viti 39 vilivyopo 11, na
meza 37 za waalimu zilizopo 13, vyumba vya madarasa 5 vilivyopo 8, nyumba za
walimu 13 zilizopo 6 pamoja na matundu 23 ya vyoo kati ya 6 yaliyopo
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi.Msangi
alieleza Gazeti hili kuwa shule inakusudiwa kufungwa kwa kukosa choo chenye
hadhi hivyo kuhofiwa wanafunzi kudumbukia wanapoenda kujisaidia
Simon Parseko (mwanafunzi) aliwaomba wadau wa elimu
wilayani Kiteto na na nje ya Wilaya kuwasaidia vitanda, magodoro na shuka kwani
wamechoka kulala chini kwa zaidi ya miaka mitano
“Mwalimu alituambia tuwaeleze wazazi wetu watununulie vitanda
ili tuje navyo hapa shuleni lakini ilishindikana kutokana na kutojua aina ya
kitanda kinachohitajika hivyo kutulazimu kuendelea kulala chini”
Naye Bakari Mahanyu ambaye ni mmoja wa maafisa wa Elimu
Wilayani hapo alitupia mpira Serkali ya Kijiji kuwa ndio wenye jukumu la
kufanya ukarabati shuleni unapohitajika
Alisema Serikali imekwisha sogeza huduma karibu na
wananchi hivyo wenye jukumu la kuendeleza shule ni pamoja na wadau wa Elimu,
wazazi pamoja na Serikali ya Kijiji na si vinginevyo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni