KCS Forum yaibua ufisadi Kiteto


KCS Forum yaibua ufisadi Kiteto
  • ·         Madiwani wadai wanapotezwa kwa kiingereza
  • ·         Wadau wazitaka mamlaka kuingilia kati kunusuru Halm

Na. Mohammed Chumvi
MTANDAO wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Kiteto (KCS Forum) Kiteto Civil Society) umeibua ufisadi Halamashauri ya Wilaya ya Kiteto hali iliyosababisha manung’uniko ya wananchi kwa kutokamilika miradi ya maendeleo pamoja na kupata hati chafu kila mara

Taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao cha wadau wa maendeleo jana imebaini kuwepo mikataba feki inayofungwa na Halamshauri na kuruhusu mianya ya ulaji dhidi ya wazabuni pamoja na tenda kutolewa kirafiki na kusababisha kushindwa kuwajibishana

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa njia ya (power Pointer) Abdul Msonde na Lilian John wajumbe wa timu ya ufuatiliaji uwajibikaji umma SAM walisema fedha zinazotolewa na Serikali hazilingani na thamani halisi ya miradi iliyopo vijijini

Pia taarifa zinazoandaliwa kwa kiswahili na kiingereza kwa walengwa zinatofautiana tarakimu za fedha jambo ambalo uwazi na ukweli unakosekana kwa watumishi wanaoandaa taarifa hizo

“Taarifa ya utekelezaji robo ya nne ya mwaka 2010//2011 inaonyesha fedha kutoka BFFS kutekeleza miradi ya maendeleo zilikuwa ni mil 342,850,000 ambapo taafifa hiyo hiyo kwa kiswahili inaonyesha mil 445,700,000 ambazo zilipangwa kwa uchimbaji visima 15,

Tofauti na Taarifa ya kiingereza inayoonyesha kuwa fedha zilipagwa kwaajili ya upimaji na usanifu wa maji vijiji 12 kazi ambayo taarifa hiyo imesema haikuonekana kimaandishi” alisema Msonde

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2011/2012 imeeleza kuwa kuna hoja za ukaguzi zenye jumla ya mil 526,179,669 ambazo Mkurugenzi alitakiwa kutafuta nyaraka zilizokosekana bila mafanikio

Pia taarifa hiyo ya CAG imeeleza kuwa kuna malipo yenye nyaraka pungufu mil 7,211,499.99, manunuzi ya shajala ambayo hayajathibitishwa mil 22,832,083, kiasi cha mil 513,613,560 zilizokusanywa na mawakala kutopelekwa Benki

Kwa upande wake Lilian John akiwasilisha taarifa ya hali halisi ya miradi iliyopo mjini na vijijini alisema kuwa miradi mingi iliyotumia fedha nyingi za wananchi imetelekezwa baada ya kutokamilika kwake huku kukikosekana jitihada za kuiboresha

“Kuna Tanki la maji lenye thmani ya zaidi ya mil 200 lililolenga kuondoa adha ya maji mjini Kibaya toka liziduliwe na aliyekuwa makamu wa Rai Alli Mohamed Shein mwaka 2009 hadi leo maji hayakuweza kuingia kama ilivyokusudiwa”alisema Lilian

Alisema mbali na mradi huo pia kuna miradi mingi ya majosho, pamoja na maji kwaajili ya Binadamu na mifugo imeteketea kwa kujengwa chini ya kiwango huku viongozi wakiwa kimya bila kutafuta ufumbuzi wake

Kwa upande wake Hassan Benzi Diwani (CCM) alisema tatizo lililopo ni kuwepo kwa madiwani ni kuwepo kwa taarifa zinazo andaliwa kwa lugha ya Kiiingereza ambayo sio rafiki kwa madiwani hivyo kujikuta wakipitisha masuala mengi bila wao kujua

Akichangia taarifa hiyo Hassani Konki (mwananchi) alisema hakuna sababu ya kuwa watumishi wasiokuwa waadilifu ndani ya Halamshauri akisema badala ya Serikali kusubiri madhara waondoke na wachukuliwe hatua juu ya ubadhirifu

“Kiteto hatuna nafasi ya kuendelea kuwa na waizi,watumishi wana nawiri,wanatakata,wanajijenga kumbe wanatuhujumu, kama kuna taarifa ya CAG inasema kuna wizi kiasi hicho muda wote wanasubiri nini”?

Naye Mashaka Saidi Fundi mwangalizi wa haki za Binadamu alisema Serikali isisubiri mwananchi ambaye kwanza uelewa wake ni mdogo achukuwe hatua na kuongeza kuwa anataka kuona viongozi wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto wanawajibika katika nafasi zao la sivyo ataenda mahakamani kumshitaki Mkurugenzi

Bakari Maunganya (mwananchi) alisema kinachosababisa kuwepo kwa matatizo ni Viongozi kulindana, akitolea mfano wa jinsi matatiozo yanavyowakumba wananchi wa kiteto kuwa kila mara wananchi wanalalamika bila hatua kuchukuliwa

Kwa upande wake Mainge Lemalali Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto kuhusu kutokamilika kwa miradi hiyo alisema ni kutokana na wanachi kushindwa kuchangia asilimia katika miradi hiyo

Kuhusu hoja za ukaguzi Lemalali alisema zipo jitihada zilizofanywa na Serikali kwa watumishi wake akisema walio onekana kuwa na matatizo yaliyozidi kiwango wamehamishwa na wengine hawatavumilika watachukuliwa hatua

Alisema Wilaya ya Kiteto sio ya majaribio tena kwani madhara makubwa yamejitokeza kwenye miradi ya wananchi na kuongeza kuna watumishi wengi wamehamishwa na wataendelea kuhamishwa kwa kutowajibika kwao

Akieleza malengo ya kikao hicho Yusuph Mohamed Mtatibu wa KCS Forum alisema ni kutoa mrejesho wa taarifa ya ufuatiliaji utelelezaji wa miradi ya maji, kilimo, na mifugo iliyotekelezwa toka mwaka 2010 hadi 2012 kazi ambayo ilifadhiliwa na Ubalozi wa Switzeland

Mwisho

Maoni