Bi. Mutagurwa aliyeingiza mikono mfukoni apata ufafanuzi kwa Oska Mwenyekiti wa Soko la Kibaya jinsi soko hilo lilivyoungua mwishoni mwa mwaka jana
Mali za wafanya biashara wa Soko Kuu la Kibaya zikiwa zinaonekana kumeteketea baada ya kuungua kwa soko hilo mwishoni mwa mwaka jana
Bi Mutagurwa akionyeshwa jinsi soko kuu la Kibaya lilivyoteketea
Soko kuu la Kibaya lilivyoteketea
Madiwani
Kiteto wavutana kuhusu ujenzi soko la Kibaya
NA. MOHAMED HAMAD
Madiwani wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani
Manyara wamejikuta katika wakati mgumu kwenye mjadala wa ujenzi wa Soko la
Kibaya lililoungua mwishoni mwa mwaka jana baada ya kila mmoja kutaka hoja yake
izingatiwe
Kaimu Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto
Rajabu Chongoe alisema Halamshauri ya Wilaya imetenga mil 100 katika Bajeti
yake kwa mwaka 2014/2015 kati ya mil 400 zinazohitajika kukamilisha soko hilo
“Wahemiwa pamoja na uhitaji soko la Kibaya kwa sasa kama
lilivyokuwa linatumika, Bajeti ya mwaka huu tumetenga kiasi cha mil 100 ambazo
tungepata Baraka kutoka kwenu zingeweza kuanza kazi mara tu baada ya kuzipata
kutoka Serikali kuu”
Wakati hayo yakielezwa hoja zilianza kwa madiwani wakisema
hicho ni kidodo huku wengine wakidai kielekezwe kwenye soko la Sunya ambalo
limetelekezwa kwa muda mrefu na wengine kudai soko hilo lisijengwe hapo
kutokana eneo hilo kuwa dogo
Hassani Benzi (CCM) Diwani wa Dosidosi akichangia hoja
hiyo alipendekeza kuwa litafutwe eneo linguine kuajili ya ujenzi huo kutokana
na kukua kwa mji na kwamba Soko linalotakiwa kujengwa ni la kisasa na ambalo
litakidhi vigezo vya masoko makubwa hapa nchini
“Sioni sababu ya kuwa na soko dogo hapo linalohitajika la
kisasa zaidi tofauti na lililokuwemo awali kwani lazima liwe na miundombinu ya
kukabiliana na majanga ya moto na kadhalika na sio kama lile lililoungua”alisema
Benzi
Nae Mussa Britoni (CCM) Diwani wa Sunya alisema kutokana
na kutengwa kiasi kidogo cha fedha hizo hazitoshi hivyo zielekezwe kwenye kata
yake ambako kuna soko la muda mrefu lililotelekezwa na halijakamilika ili
zisaidie wananchi hao
Kwa Upande wake Mwasigwa Kimosa aliwataka wataalamu kutafuta eneo mbadala
katika mji wa Kibaya ambalo fedha hizo zitaelekezwa hapo kwaajili ya ujenzi wa
awali ili mwaka mwingine watenge kiasi kingine cha fedha kukamuilisha Soko hilo
Hadi hoja hiyo inafungwa hakuna jibu la moja kwa moja
lililopatikana kuhusu hatma ya soko hilo
na kwamba wafanya biashara hao wamebaki njia panda kwa kutojua lini soko hilo
litajengwa na wapi ili waweze kuendelea na biashara zao
Hata hivyo Mainge Lemalali Mwenyekiti wa Halamshauri ya
Wilaya ya Kiteto akihitimisha hoja hiyo alisema kiasi hicho ni kidogo na
tegemeo la Halamshauri ni kupata fedha kutoka Serikali Kuu ambao nao huchelewa
kutoa
“Fedha nyingi ni kutoka kwa wafadhili ni mpaka walete kwa
hiyo hata kama tutavutana haina maana lazima tuwe wapole kwa wazungu ambao ndio
wanachangie bajeti zetu kiasi kikubwa kutekeleza miradi ya maendeleo”alisema
Mainge
Kuungua kwa soko kuu la mji wa Kibaya kumesababisha
hasara ya zaidi ya mil 56 na kwa sasa wafanya biashara wanauzia bidhaa zao
juani na wengine kwenye vibada vya kienyeji hali inayowapa usumbufu mkubwa
katika kazi hizo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni