MTOTO ALIYENG’ATWA NA MBWA KITETO AFARIKI

NA Mohamed Hamad
SIKU moja baada ya DIRA kutangaza juu ya mtoto Mgano Koronyo (3) wa Ndaleta Wilayani Kiteto aliyecheleweshwa kupata tiba baada ya kung’atwa na mbwa mwenye kichaa na kuelezwa na daktari kuwa jitihada za kumwokoa zimegonga mwamba, amefariki Dunia 

Hayo yameelezwa na familia ya motto huyo ambayo wako kwenye mazishi ya motto huyo wakisema hawakuwa na njia mbadala dhidi ya kusubiri kudra za mungu kuokoa maisha ya motto huyo

Akizungumza hayo baba wa motto huyo amesema awali walielezwa na daktari kuwa hatua aliyokuwa amefikia motto wake ilikuwa ya mwisho baada ya kushindwa ula wala kunywa huku akitapatapa ikielezwa kuwa tarari alikwisha pata kichaa cha mbwa

Marehemu Mgano aliwaliza umati wa wananchi wa kibaya waliofika kumwona akilia kwa sauti kubwa ya masikitika akidai kwenda nyumbani hali iliyomfanya Dr Malisa kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya kuwaruhusu kwenda nyumbani kabla ya kifo hicho

Awali motto huyo alichomwa sindano ya tetenasi badala ya ile ya kichaa cha mbwa katika Zahanati ya njoro kwa maksudi ya Dr huyo kasha kutokomea na tsh 90,000 ikidaiwa kuwa hiyo ndio Dozi ya ugonjwa alioupata

Hata hivyo mzazi wa motto huyo ameomba Serikali kufuatilia juu ya tukio hilo akisema limesababisha apoteze motto wake huyo wa kiume kwa maksudi kwa kuendekezwa fedha kuliko kutibu mgonjwa

Kwa mujibu wa Dr Malisa amesema hatua za awali alizofanya ni kumwita Dr huyo aliyefahamika kwa jina moja la Stive na kuanza kumhoji na kwamba baada ya kifo hicho amesitisha zoezi hilo hadi jumatatu ambapo ataendelea na zoezi lake hilo

mwisho

Maoni