CCM KITETO YAMEGUKA VIPANDE
NA.MOHAMED HAMAD
UONGOZI wa chama cha mapinduzi CCM wilayani kiteto umeingia katika malumbano hali iliyodaiwa kuwa chama kimegawanyika vipandevipande na kuhofiwa kuwepo kwa anguko kubwa 2015
Taarifa za uhakika ndani ya chama hicho zimeeleza kuwa malumbano hayo yametokana na umoja wa vijana UVCCM kuhitilafiana na Mbunge wao Benedict Ole Nangoro ambaye kwa sasa amelazimika kuomba nguvu Mkoani kurejeshewa nafasi yake ya ukamanda
Awali imeelezwa kuwa kuwalikuwa na nafasi ya ukamanda ambayo aliishikilia Mbunge Nangoro kwa miaka kadhaa na baada ya muda wake kwisha alihitaji tena jambo ambalo vijana hao waliona hana sifa hiyo
Uongozi wa Mkoa uliteua jina la Mhe. Nangoro kuwa kamanda wa vijana wa Wilaya ili aje kuthibitishwa kwenye baraza la vijana la wilaya ambapo ilishindikana baada ya madai ya vijana hao kuwa Mb. Wao huyo hana maslahi kwao
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa UVCCM wilaya Emmanuel Keyaa akizungumza na Blog hii alisema maamuzi yaliyofanywa na baraza la vijana mei mwaka huu 2014 yalikuwa sahii kutokana na madai mbalimbali ya vijana hao
Alisema Mb.Nangoro amekuwa akilalamikiwa juu ya msaada wa vyerehani kumi viliotolewa na Mhe Mery Nagu miaka miwili iliyopita na hakuwa tayari kuvitoa hali iliyowafanya vijana kuchukizwa na kitendo hicho
Pia wamedai kuwa kwa kipindi cha vurugu kati ya wakulima na wafugaji Mbunge Nangoro alipaswa kuwa mstari wa mbele kukutanisha makundi hayo ili yasiweze kuleta madhara badala yake alishindwa hata kutoa pole kwa familia za watu waliopoteza maisha
“Kilichosikitisha sana ni kutomwona Mbunge wetu kwenye shida iliyojitokeza toka mapema mwaka huu ya watu kuuana ambapo zaidi ya watu kumi walipoteza maisha na hakuweza kusikika hata akilaani mauaji hayo tofauti na wawakilishi wengine”alisema
Katika hitimisho la mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya alisema kwakuwa umoja wa vijana wa mkoa wa manyara unalazimisha Mbunge Nangoro awe kamanda wa vijana wilaya ya Kiteto atatambulika kwa mkoa tu na sio wilayani
Siwezi kuwa na kamanda ambaye hatokani na ridhaa ya wajumbe wangu ambao ni baraza vijana wa CCM na kwa hivi karibuni kilichofanyika nikulazimishwa maamuzi ya kumkubali nasema hana nafasi mpaka pawepo na maamuzi ya vijana na kwa vikao halali na si vinginevyo
“Nililazimika kutoka nje ya kikao na katibu wangu kwani kilichokuwa kinalazimishwa ni kutaka kufanyike maamuzi mengine mbadala ikielezwa kuwa eti kuna vifungu vilikosewa lakini lengo n kumrejesha Mbunge Nangoro nafasi ya ukamanda”alizidi kusema Keyaa
Bado swala hili ni gumu sana kuna haja ya mbunge huyu kufikiri kwa makini juu ya uamuzi uliofanywa na vijana na kama kuna haja ya yeye kung’ang’ania nafasi hiyo basi itaeleweka zaidi baadaye alimalizia mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Blog hii ilizungumza na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa ambaye alisema hajafika kiteto kutengua maamuzi ya vijana bali alitaka kuwakumbusha baadhi ya kanuni ambazo zimekiukwa
“sijaja kiteto kutengua maamuzi ya vijana na wala kwa aliyekuambua nimekuja kufanya hivyo aendelee kukupa habari zaidi na wala sihitaji habari zetu zitangazwe kwenye vyombo vya habari”alimalizia na kukata simu mwenyekiti huyo
ITAENDELEA …….
Maoni
Chapisha Maoni