KITETO YAZINDUA TASAF AWAMU YA TATU 2014

MKUU WA WILAYA YA KITETO MARTHA JAKI UMBULA KATIKA UZINDUZI WA TASAF AWAMU YA TATU -KITETO 2014
MRATIBU WA TASAF WILAYA ROSEMERY GARIBONA AKIWA KATIKA UZINDUZI WA TASAF AWAMU YA TATU KITETO 2014


DC Kiteto awataka wananchi kulinda amani

Na Mohamed Hamad
MKUU wa wilaya ya Kiteto Martha Jaki Umbula amewataka wananchi wilayani humo kulinda amani ambayo ilianza kutoweka kutokana kwa kuibuka migogoro ya ardhi ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji

Akizungumza hayo kwenye uzinduzi wa TASAF awamu ya tatu jana mkuu huyo wa wilaya amesema amani ikitoweka hata utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi inakuwa vigumu

“Huwezi kupeleka mradi eneo ambalo halina usalama, hivi karibuni wilaya yetu ilikumbwa na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji hali iliyoleta taswira mbaya kwa watu kuuana”

“Niwaombe wananchi kwa kila mmoja ulina amani ambayo ikitoweka hakuna anayeweza kufanya maendeleo yoyote na kwamba TASAF awamu ya tatu itafanikiwa tu endapo amani hii ikiendelea kutawala”alisema Umbula

Kwa upande wake Chamila Bidya mmoja wa maafisa wa mradi wa jamii TASAF Taifa akiwasilisha mpango na taratibu za utekelezaji wake alisema jula ya vijiji 37 Wilayani humo vitanufaika na TASAF awani ya tatu

Alisema awamu ya tatu ya TASAF imejielekeza zaidi katika kusaidia kaya maskini tofauti na awamu ya pili ambayo ilijiielekeza katika kusaidia miradi ya jamii kama afya,elimu na miundombinu

Wakichangia hoja hiyo baadhi ya wajumbe walikosoa utaratibu huo wakidai kuwa hautakuwa na tija kusaidia mtu mmojammoja  na badala yake manufaa yangepatikana tu kwa kuanzisha miradi ya jamii
“Haya hiyo 8,500 kwa mlengwa haina maana kwakuwa huduma za jamii zenyewe hazipo kwa kiwango stajili kwani elimu,afya,vyote vinahitaji kugharamiwa hivyo kiasi hicho kilichotajwa kwa mtu maskini hakitosho”alisema Ibrahimu Ole Mario katibu Tarafa Tarafa ya makami

Mwisho



Maoni