Mwalimu
mbaroni kwa kujihusisha mapenzi na mwanafunzi
Na Mohamed Hamad
JESHI la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara
linamshikilia mwalimu Abubakar wa Kiteto Sekondari kwa tuhuma za kufanya
mapenzi na mwanafunzi wakiwa nyumbani kwao usiku wa kuamkia julay 19 mwaka huu
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea kwa mwanafunzi wa kike jina limehifadhiwa kuendelea kufanyiwa vipimo
huku mahojiano kwa mtuhumiwa yakiendelea
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa siku hiyo mwalimu
alifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo majira ya usiku wa manane ambapo ndugu
walimfumania kisha kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi Kiteto
“Kwa kweli hata kama ni masomo hayakupaswa kufanywa
nyakati hizo kwani ule ulikuwa ni muda wa kulala sanane za usiku, tunatarajia
kuona sheria ikichukua mkondo wake lakini pia huo ni ukosefu wa maadili ya
kitaaluma kwa mwalimu huyo”alisema mmoja wa mashuhuda
Hata hivyo MTANZANIA jumapili iliweza kumwona mwalimu
huyo akifanyiwa mahojiano kituo cha polisi Kiteto juu ya tukio hilo ambapo kwa
taarifa za awali imeelezwa kuwa baada ya ripoti ya Hospitali kupatikana hatua
zaidi zitajulikana
Kwa upande wake John Kimaro mkuu wa shule ya Kiteto
Sekondari alieleza kuwa amesikitishwa na kitendo hicho akisema tuhuma hizo
zinachafua kada ya ualimu na kwamba anawaweka pabaya walimu wenzake
“Binafsi nililazimika kutoa taarifa hivi karibuni kwa
mwajiri juu ya nyendo za mwalimu huyu nilitegemea hatua zingechukuliwa lakini
hata hivyo nadhani kwa hili hata kama hahusiki ama anahusika lazima mwajiri
aone kwa undani juu ya mwenendo wa mwalimu huyu”alisema Kimaro
Kwa upande wa familia ya mwanafunzi wameitaka Serikali
kuchunguza suala hili kwa kina ili kutokomeza vitendo hivi na kama wataviachia
madhara makubwa yanaweza kujitokeza siku za usoni kwa jamii kuamua kuchukua
hatua badala ya kuiachia polisi
Nae mjumbe wa bodi Mashaka Saidi Fundi ambaye pia ni
mwangalizi wa haki za binadamu Wilayani Kiteto amelitaka Jeshi la Polisi
kufanya kazi zake kwa uadilifu kuchunguza ili kubaini kilichotokea ili sheria
iweze kufuata mkondo wake na kwamba vitendo kama hivyo viweze kutokomeza
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni