Wajawazito
Kiteto walalamika huduma mbovu
NA Mohamed Hamad MANYARA
AKINAMAMA wajawazito wilayani Kiteto mkoani Manyara
wameingia katika malumbani na uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Kiteto baada ya kutozwa Tsh
30,000 wakati wa kujifungua
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema pamoja na kutozwa fedha hiyo hawapati
risiti kuhalalisha malipo yao jambo ambalo linawapa hofu kuwa wanahujumiwa huku
Serikali ikisema huduma hiyo ni bure
“Mama mjamzito akifika hospitali analazimika kutalipa
kila kitu kuanzia kadi vipimo pamoja na vifaa vyote vinavyohitajika wakati
Serikali imetangaza kuwa huduma hiyo ni bure hali inayoleta usumbufu”alisema mmoja
wa akinamama hao
Alisema pamoja na kutolewa taarifa kwa viongozi wanao
husika wa Hospitali hiyo huambulia kauli za kuwa “hiyo ndio Serikali yenu
lazima mchangie na hakuna dawa za bure ”hivyo hali hiyo inatofautiana na kauli
ya Serikali kuwa huduma hiyo ni bure
Kwa upande wa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto
wakizungumzia sakata hili walisema kuna upungufu wa dawa katika Hospitali na
kwamba ili kukabiliana na tatizo hilo wananchi wanatakiwa wajiunge na mfuko wa
jamii CHF
“Swala hili linafahamika nchi nzima kwamba Serikali haina
fedha pamoja na kupata dawa kutoka MSD bado tuna tatizo la kutokidhi dawa hizo
kwa wananchi hii inatokana na wengi wao kuto jiunga na mfuko wa afya”alisema Dr
Joseph Tutuba mganga mkuu wa hospitali hiyo
Aliwataka wananchi Wilayani humo kujiunga na mfuko huo
ambao utakuwa na msaada mkubwa kwao na kwamba kila mtu aliyejiunga atapata
huduma hiyo kwa wakati na pia dawa hazitakosekana
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni