Wakulima
Kiteto wahofu kutouza mazao yao Serikalini
Na.Mohamed Hamad Kiteto
Hofu ya wakulima kutouza mazao yao imetanda wilayani
Kiteto Mkoani Manyara baada ya Serikali kutangaza kuwa ina uwezo wa kununua tani
elfu moja sawa na gunia elfu kumi huku kukiwa na hitaji kubwa la wakulima
kutaka kuuza mazao yao
Serikali kupitia kitengo cha National Food Reserve
Authority cha Dodoma (NRFA) imeamua kuweka kambi kijiji cha Engusero ya kununua
mazao hayo aina ya mahindi kwa wakulima ili kuwapunguzia adha ya kulanguliwa
Hata hvyo gazeti hili lilifika kituoni hapo na kuongea na
wakulima ambao walisema kuna changamoto katika zoezi hilo zikiwemo rushwa
pamoja na utaratibu mbobu wa kupokea mazao hayo
Walisema Serikali kutangaza kununua tani elfu moja inasababisha
kuwepo kwa hujma mbalimbali hali
inayofanya wakulima wadogo kushindwa kuuza mazao yao kwenye soko hilo hivyo kutekwa
na wafanya biashara wakubwa
Kilo moja ya mahindi inanunuliwa kwa sh 500 tofauti na
soko la Kibaigwa lililopo Kongwa hivyo kufanya
soko hilo kutekwa na wafanya biashara hao wakubwa kutoka ndani na nje ya wilaya
ya Kiteto huku rushwa ikidaiwa kushamiri
Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya Engusero Leonard Kunamila
amewahakikishia wakulima hao kuwa atapambana na urasimu huo na kwamba kila
mmoja atauza mazao yake hadi hapo Serikali itakapositisha kununua mazao hayo
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Engusero Haji Bundala
ameitaka Serikali kuongeza fedha ili kukidhi mahitaji ya wakulima kuuza mazao yao kwa bei hiyo kwa kuwa imekuwa
na tija kubwa hivyo wengi wao watanufaika
“Hapa tuna makundi mengi ya wakulima wapo waliokopa fedha
benki kwaajili ya kufanya kazi ya kilimo ambapo sasa wanadaiwa na njia pekee ni
kuuza mazao yao ili walipe madeni na sio vinginevyo”
Lakini pia wapo wanaofanya kazi yao ni kilimo kama sehemu ya kuendesha maisha yao hao
wapo pamoja na wafanya biashara wanatakiwa kunufaika na bei hii ambayo kwa sasa
itakuwa na tija kuliko kulanguliwa na wafanyabiashara”alisema akisisitiza
Iko haja ya Serikali kuongeza fedha za kutosha ili iweze
kununua mazao haya ambapo hadi sasa kuna zaidi ya gunia elfu kumi zaidi ya
lengo la Seriali huku wakulima wakiwa wametumia gharama kubwa kuleta bidhaa zao
Wakati huo wakulima hao wameitaka Serikali Wilayani
Kiteto pamoja na uongozi wa juu kufika katika soko hilo kuona changamoto
zinazowakabili na ambazo zinadaiwa kama hazitatatuliwa zinaweza kuzoroteza
zoezi hilo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni