KINNAPA
latimiza ndoto za kamati za shule Kiteto
Na. Mohamed Hamad MANYARA
SHIRIKA lisilokuwa la
kiserikali la KINNAPA wilayani Kiteto mkoani Manyara limetimiza ndoto ya baadhi
ya kamati za shule za msingi kwenda ziara ya kimafunzo Kibaha mkoani Pwani ili
ziweze kujua majukumu yao
Akieleza kazi zinazofanywa
na shirika mbele ya wajumbe wa kamati za shule za msingi wilayani Kiteto na
Kibaha ya Pwani mratibu wa kitengo cha elimu Shirika la KINNAPA Ngaringe Maitey
alisema kuwa ni pamoja kuboresha usafi na mazingira kwenye shule na zahanati
(wash project}
Kuhakikisha upatikanaji wa
mali elimu bora na kujenga uwezo kwa wananchi (Kiteto livelihood support)
Kuhakikisha ushiriki wa jamii katika miradi ya umma kufuatilia kusimamia
kutathmini matumizi ya mali za umma (Public accounterbility)
Nyingine ni mwanzo bora
(nutrition),(small holder group development) kuongeza uzalishaji wa zao la
mahindi kwa wakulima wadogo Kiteto,pamoja na kuboresha ulinzi wa nyanda za juu
za lalisho ya mifugo
“Baadhi ya wajumbe wa kamati
za shule za msingi hawajui mjukumu yao ipasavyo hali inayofanya elimu kudorora na
kusababisha manung’uniko makubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao iliyopo
madarakani”
“Hatufanyi kazi za KINNAPA bali
tunatekeleza majukumu ya Serikali, kila mtu ana wajibu wa kufanya kazi kwa
ufanisi na katika hatua hiyo KINNAPA tunazijengea uwezo kamati za shule ili
ziweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo”alisema Ngaringe
Kwa upande wake Melubo Ole
Naiganya mwenyekiti shule ya msingi Irkiushibour alisema, awali hakuwa
anafahamu majukumu ya kamati za shule hivyo kushindwa kutimiza wajibu wake na
kusababisha shule kudhorota kielimu
Alisema elimu aliyoipata
kutoka shirika la KINNAPA pamoja na ziara ya kimafunzo shule ya msingi Tumbi
iliyopo Kibaha mkoani Pwani atahakikisha anatimiza wajibu wake kulinda shule
yake kwa kusimamia miradi na kubuni…mingine
“Sikuwa najua kitu pamoja na
kwamba wazazi waliona nafaa kwa kunichagua ili kushika wadhifa huo toka mwaka
2013 lakini baada ya kujegewa uwezo naamini kuwa nitawajibika ipasavyo katika
nafasi hii ili nilete tija kwa shule yangu”alisema
Naye Mwenyekiti wa shule ya
msingi Engusero engine Wilbrod Mathayo alisema ataiga mafanikio aliyoyaona shule
ya msingi Tumbi ambayo yamesababishwa na umoja wa kamati hiyo ambayo imekuwa ya
kuigwa
“Najua kuna kazi kubwa
iliyofanyika hapa Tumbi na ndio maana tumeona mambo mengi mazuri hivyo naahidi
katika shule yangu changamoto zilizopo nazibadilisha kuwa fursa ya kujiletea
maendeleo kwa wananchi wangu”alisisitiza
Awali akieleza mafanikio ya
shule hiyo Khamis Mbonde mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Tumbi alisema
siri ya mafanikio ya shule yake ni pamoja na kuwepo kwa mipango imara
inayoungwa mkono na wazazi katika utekelezaji
“Kabla ya kufanya jambo
lolote hapa shuleni kwanza tunashirikisha wazazi ambao wao ndio wenye uchungu
na shule hii hivyo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wala hatuwalazimishi kwa
jambo lolote” alisisitiza Mbonde
Mwalimu mkuu wa shule hiyo
bw Jani Moses alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa na shule yake bado anahitaji
shirika la KINNAPA kuona namna ya kusaidia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika
shule yake kwakuwa ni shirika
Alisema shule yao
inakabiliwa na uhaba wa madawati vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za
waalimu hivyo wangependa kuona shirika la KINNAPA lililoweka ubia na wao lione
namna ya kusaidia changamoto zilizopo
Mwisho
KINNAPA
latimiza ndoto za kamati za shule Kiteto
Na. Mohamed Hamad MANYARA
SHIRIKA lisilokuwa la
kiserikali la KINNAPA wilayani Kiteto mkoani Manyara limetimiza ndoto ya baadhi
ya kamati za shule za msingi kwenda ziara ya kimafunzo Kibaha mkoani Pwani ili
ziweze kujua majukumu yao
Akieleza kazi zinazofanywa
na shirika mbele ya wajumbe wa kamati za shule za msingi wilayani Kiteto na
Kibaha ya Pwani mratibu wa kitengo cha elimu Shirika la KINNAPA Ngaringe Maitey
alisema kuwa ni pamoja kuboresha usafi na mazingira kwenye shule na zahanati
(wash project}
Kuhakikisha upatikanaji wa
mali elimu bora na kujenga uwezo kwa wananchi (Kiteto livelihood support)
Kuhakikisha ushiriki wa jamii katika miradi ya umma kufuatilia kusimamia
kutathmini matumizi ya mali za umma (Public accounterbility)
Nyingine ni mwanzo bora (nutrition),(small
holder group development) kuongeza uzalishaji wa zao la mahindi kwa wakulima
wadogo Kiteto,pamoja na kuboresha ulinzi wa nyanda za juu za lalisho ya mifugo
“Baadhi ya wajumbe wa kamati
za shule za msingi hawajui mjukumu yao ipasavyo hali inayofanya elimu kudorora na
kusababisha manung’uniko makubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao iliyopo
madarakani”
“Hatufanyi kazi za KINNAPA bali
tunatekeleza majukumu ya Serikali, kila mtu ana wajibu wa kufanya kazi kwa
ufanisi na katika hatua hiyo KINNAPA tunazijengea uwezo kamati za shule ili
ziweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo”alisema Ngaringe
Kwa upande wake Melubo Ole
Naiganya mwenyekiti shule ya msingi Irkiushibour alisema, awali hakuwa
anafahamu majukumu ya kamati za shule hivyo kushindwa kutimiza wajibu wake na
kusababisha shule kudhorota kielimu
Alisema elimu aliyoipata
kutoka shirika la KINNAPA pamoja na ziara ya kimafunzo shule ya msingi Tumbi
iliyopo Kibaha mkoani Pwani atahakikisha anatimiza wajibu wake kulinda shule
yake kwa kusimamia miradi na kubuni…mingine
“Sikuwa najua kitu pamoja na
kwamba wazazi waliona nafaa kwa kunichagua ili kushika wadhifa huo toka mwaka
2013 lakini baada ya kujegewa uwezo naamini kuwa nitawajibika ipasavyo katika
nafasi hii ili nilete tija kwa shule yangu”alisema
Naye Mwenyekiti wa shule ya
msingi Engusero engine Wilbrod Mathayo alisema ataiga mafanikio aliyoyaona shule
ya msingi Tumbi ambayo yamesababishwa na umoja wa kamati hiyo ambayo imekuwa ya
kuigwa
“Najua kuna kazi kubwa
iliyofanyika hapa Tumbi na ndio maana tumeona mambo mengi mazuri hivyo naahidi
katika shule yangu changamoto zilizopo nazibadilisha kuwa fursa ya kujiletea
maendeleo kwa wananchi wangu”alisisitiza
Awali akieleza mafanikio ya
shule hiyo Khamis Mbonde mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Tumbi alisema
siri ya mafanikio ya shule yake ni pamoja na kuwepo kwa mipango imara
inayoungwa mkono na wazazi katika utekelezaji
“Kabla ya kufanya jambo
lolote hapa shuleni kwanza tunashirikisha wazazi ambao wao ndio wenye uchungu
na shule hii hivyo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wala hatuwalazimishi kwa
jambo lolote” alisisitiza Mbonde
Mwalimu mkuu wa shule hiyo
bw Jani Moses alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa na shule yake bado anahitaji
shirika la KINNAPA kuona namna ya kusaidia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika
shule yake kwakuwa ni shirika
Alisema shule yao
inakabiliwa na uhaba wa madawati vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za
waalimu hivyo wangependa kuona shirika la KINNAPA lililoweka ubia na wao lione
namna ya kusaidia changamoto zilizopo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni