KINNAPA NA MKAKATI WA KUBORESHA ELIMU KITETO



KINNAPA na mkakati wa kuboresha elimu Kiteto

Na. Mohamed Hamad Manyara
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la KINNAPA wilayani kiteto mkoani Manyara katika kitengo chake cha elimu, limeanza kuzijengea uwezo kamati za shule za msingi ili kujua majukumu yao

Jumla ya wajumbe 40 kutoka vijiji 20 vya Partimbo,Kaloleni,Matui, Engusero engine,Ndirigish, njia panda, Dosidosi,Ormaroroi,Ilkiushbaour,Lesoit,orgine, Emart,Makami, Ngabolo,Njoro,Orpopong’I

Vijiji vingine ni pamoja Ilera,Mbigir, Lerug,Kijungu, ambao kwa pamoja wanaendelea kujengewa uwezo na shirika hilo ili waweze kutenda majumu yao wanapokuwa mahali pa kazi

Akieleza malengo ya mafunzo hayo mratibu wa kitengo hicho bw. Ngaringa amesema uchunguzi  uliofanywa  na shirika hilo umebaini kuwa wajumbe wengi wa kamati za shule wilayani humo hawajui wajibu wao

Alisema kutojua wajubu wao kumechangia kushusha kiwango cha elimu hasa pale wanaposhindwa kuhoji,kusimamia majukumu waliopewa na wananchi shuleni

“Tumeona kuwa kuna haja ya kutoa elimu kwa kamati ili waweze kujua wajibu wao wanapokuwa katika majukumu yao mara baada ya kuchaguliwa na wananci katika nafasi hizo”

Amesema njia pekee ya kuinua kiwango cha elimu wilayani Kiteto ni kuwajengea uwezo wadau wa elimu ili waweze kusimamia shule zao ipasavyo wakiwemo waalimu wakuu waratibu wa shule pamoja na kamati zenyewe

Hata hivyo changamoto kubwa zimeelezwa kujitokeza katika kuboresha elimu ya msingi ambazo zimechangiwa na ukosefu wa uwajibikajipamoja na elimu duni kwa wajumbe ama viongozi waliopewa mamlaka

Wajumbe hao wamezitaka mamlaka zinazohusika na elimu ikiwemo Serikali na mashirika ya umma kuendelea kuzijengea uwezo kamati za shule ili ziweze kutenda majukumu yao ipasavyo

Mwisho

Maoni