Zaidi
ya Bunduki 200 zakamatwa Kiteto
Na. Mohamed Hamad Kiteto
Matukio ya kihalifu yanayoendelea kujitokeza wilayani
Kiteto mkoani Manyara yamelazimu Jeshi la Polisi wilayani humo kukusanya silaha
aina ya bunduki zinazomilikiwa kihalali na isivyo halali ili kubaini zilizotumika
kufanya uhalifu
Zaidi ya bunduki 200 za aina tofauti zikiwemo
Raifo,Shotigan,na Magobole zimekusanywa wilayani humo kwa lengo la kufanya
uchunguzi kama zimehusika katika mauaji ya watu saba yaliyotokea hivi karibuni
katika vijiji vya Chekanao na Matui
Awali akizungumza na vyombo vya habari Deosdedit Nsimeck
Kamanda wa Polosi wa Mkoa wa Manyara mjini Kibaya alisema hatua hiyo inasaidia
kubaini silaha zinazofanya matukio ya kihalifu
katika maeneo mbalimbali Wilayani humo
“Silaha hizo toka kwa wananchi tumeamua kuzikusanya
zikiwemo zile zinazomilikiwa kihalali na isivyo halali ili kudhibiti vitendo
vya kihalifu vinavyoendelea kujitokeza vikiwemo vya mauaji ya mara kwa mara”alisema
Nsimeck
Wananchi na viongozi katika maeneo tofauti wamepongeza
kitendo hicho wakisema hatua hiyo ni busara iliyotumika ambayo itakomesha
mauaji pamoja na kuwepo kwa changamoto kubwa katika kuzipata huko vijijini
“Wakati mwagine mmiliki wa Silaha husika kihalali
analazimika kuingia mitini akiwa hana nia ya kuikabidhi lakini baadaye
anaagizia mke wake kwenda kuikabidhi kutokana na sababu zao mbalimbali” alisema
mmoja wa maafisa hao
Kwa upande wake Emanuel Papian mjumbe wa NEC (CCM) Taifa
akizungumzia hatua hiyo alisema matukio hayo yatapungua kutokana na jitihada hizo na kulitaka Jeshi la
Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani
“Utakuta mhalifu anafanya atakavyo mf. mauaji yanayo
endelea kutokea Kiteto hutasikia aliyefanya matukio anawajibishwa, na hili
linaenda sambamba na kutowajibika kwa viongozi wa ngazo mbalimbali za maamuzi”alisisitiza
MNEC huyo
Katika hatua hiyo mjumbe huyo aliwataka wananchi Wilayani
Kiteto kujipima kama wanatosha katika nafasi wanazoshikilia ili kuepusha
manunguniko kwa wananchi ambayo yanajitokeza kila mara
Natamani siku moja nisikie na kuona wananchi wa Kiteto
wanaishi kwa amani na kujivunia viongozi wao waliowachagua kuwa wanasikilizana
katika shuhuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni