Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian akiwa katika picha ya pamoja na na jamii ya kifugaji wamasai hivi karibuni kata ya matui wilayani Kiteto
Kiteto
yatakiwa kujengwa upya
Na. Mohamed Hamad Manyara
MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian
amevunja ukimya na kusema wilaya ya Kiteto inatakiwa kujengwa upya kwa misingi
ya watu kupendana, kuondoa chuki,ubaguzi wa kikabila,rushwa na ubinafsi
Akizungumza hayo mjini kibaya MNEC huyo hivi karibuni
alisema wakulima na wafugaji wanachuki dhidi ya baadhi ya viongozi wa Serikali
kutokana na kutotatuliwa matatizo yao kwa muda mrefu
“Huwezi kuamini hatua iliyofikiwa na wananchi wa kiteto
ni kuuana kwa kuchinjana,kupigana risasi,kukatana mapanga hadi kufa na hii ni
kutokana na kukosekana kwa usimamizi mzuri wa ardhi”
Alisema pamoja na kuwepo kwa sheria ya ardhi ambayo
inatakiwa kusimamiwa na viongozi waliopo madarakani tatizo lililopo ni
kukosekana kwa uadilifu dhidi ya baadhi ya viongozi wa Serikali hivyo
kuwagombanisha wananchi hao
“Utamkuta kiongozi anawezo wa kuongea na kundi moja tu la
baadhi ya wananchi wake huku wengine wakitengwa hali hii inachangia sana
mgogoro huu na ilipigwa vikali na Baba wa Taifa letu mwalimu Nyerere”alisema
Papian
Akitoa suluhisho la mgogoro huo wa Kiteto alisema njia
pekee ya kukabilia tatizo hili ni viongozi kuacha tabia za kuongoza kwa misingi
ya ubaguzi hasa kwa wengine kuitwa wazawa na wengine wahamiaji
Nchi ya Tanzania imejengwa kwa misingi ya umoja udugu na
mshikamano kazi ambayo ilifanywa vizuri sana na mwasisi wetu baba wa taifa
lakini leo utasikia Kiongozi anasimama jukuwaani akiwaita watanzania wenzake
kuwa ni wavamizi,
“Mtu hawezi kuwa mvamizi ndani ya nchi yako kwani kila
mtu ana haki ya kuishi mahali popote ilimradi asivunje sheria, sasa hili
limegawa wananchi na kujiona kuwa wanahaki ya kuchukua hata sheria mikononi
kama kuua wenzao”
Alisema unaweza kuona mtu anaamua kumchinja mwenzake kasha
mwisho wa siku unasikia waliouawa ni watu wa kuja sio wenyeji Serikali inaliona
naiomba sheria ifuate mkondo wake na tuwe wazalendo”alisisitiza
Naamini kuna kazi kubwa inayofaywa na Serikali ikiwemo
kubaini mipaka,kutenga maeneo ya matumizi bora ya ardhi pamoja na kuongeza
vituo vya polisi “wananchi tumieni nafasi hiyo kuhakikisha tunaijenga Kiteto upya
na viongozi tuongee na makundi yote ndani ya jamii na sio kuwatenga”alisema
Papiani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni