Makamu mwenyekiti wa
Halmasauri ya wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel akifafanua jambo kwenye
kikao cha baraza la madiwani pembeni yake ni Bosco Ndunguru DED Kiteto
Manyara Picha na Mohamed Hamad
Tume:
Kiteto wekeni mabango kwenye hifadhi
Na. Mohamed Hamad Manyara
Tume maalumu toka ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasili Kiteto
mkoani manyara kushughulikia migogoro ya ardhi imeutaka uongozi wa wilaya
kuweka mabango kwenye maeneo yaliyopangwa matumizi bora ya ardhi
Hayo yameelezwa na kiongozi wa tume hiyo hakutaka jina
kutajwa akizungumza na Jambo leo kuhusu hatua iliyofikiwa na tume iliyodaiwa
kuwa itafanya kazi kwa miezi miwili na
nusu kuhakikisha migogoro imamalizika
“Kazi ya kuhakiki mipaka ya Hifadhi ya Emboley Murtangos
kwa hatua ya kwanza na ya pili imekamilika,tunataka Halmashauri iweke mabango kuonyesha
hifadhi hiyo kuepuka watu kuingia na kufanya kazi za kibinadamu” alisema
Kiongozi huyo
Pia alisema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanikiwa kwa
kiwango kizuri zaidi aliitaka Halamshauri ya Wilaya kutengeneza mkuza (barffer
zone) utakaosaidia kutenganisha eneo hiyo na maeneo mengine ambayo yamepakana
Hata hivyo kucheleweshwa kuwekwa mabango hayo kunahofiwa
kuwa watu wataweza kuingia kinyemela kwenye maeneo hayo yaliyotengwa na kufanya
shuhuli za kibinadamu kazi ambayo imepigwa marufuku
“Kwa sasa hatakiwe kuwepo mkulima wala mfugaji kwenye
Hifadhi ya Emboley Murtangos Serikali imeamua kurejesha eneo hilo katika uoto
wake wa asili kwa kutoona shughuli zozote za kibinadamu humo”alisema kiongozi
huyo
Awali baadhi ya Viongozi wilayani Kiteto walieleza
wananchi kuwa eneo hilo ni kwaajili ya hifadhi ambayo wafugaji wanaweza
kuingiza mifugo yao humo na kutoka jambo ambalo lilizu mgogoro hivyo wakulima
nao wakaamua kuingia kwa nguvu na kuanza kulima
“Tumeweka taratibu zote za kitaalamu humo eneo sasa
linafahamika na kutambulika kilichobakia ni kusimamia sheria ipasavyo na hapo
ndiko kwenye matatizo kwa baadhi ya viongozi mbalimbali hapa nchini kushindwa
kuwajibika”alisisitiza
Serikali imetumia fedha nyingi kutuma wataalamu 27 wa fani
mbalimbali kufanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili kama kutakosekana dhamira safi kusimamia kazi hii matatizo haya
yataendelea kujirudia alisisitiza kiongozi huyo
Baadhi ya wananchi wilayani hapo waliitaka Serikali
kuhakikisha kazi hiyo inakamilika mapema sambamba na kuwekwa alama za mabango
makubwa ili yabainike wasiweze kuingia ndani ya maeneo ambayo hayaruhusiwi na
yanaweza kuleta migogoro
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni