KAMATI YA PINDA YAANZA KAZI KITETO


Kamati maalumu iliyoundwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda kusuluhisha mgogoro wa wakulima na wafugaji Kiteto Picha na Mohamed Hamad Manyara





Kamati ya Pinda yaanza kazi rasmi Kiteto

Na. Mohamed Hamad Manyara.
Kamati iliyoundwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda kwaajili ya kusuluhisha mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto mkoani Manyara, imeanza kazi rasmi ya kukutanisha makundi mbalimbali ndani ya kijamii hiyo

Makundi yaliyokutaniswa ni pamoja na  wachungaji,mapadre,mashekh,viongozi wa kisiasa (Mbunge),viongozi wa kiserikali akiwemo Mkuu wa wilaya, mkurugenzi, na wakuu wa Idara  ambapo wamedai kuwa  watakutana na wananchi katika mikutano mikuu ya vijijini

Akizungumza na waadishi wa habari Askofu Amos Mhagachi wa kanisa la … ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo jana alisema jukumu la kukabiliana na migogoro ya ardhi ni la wadau wote wa maendeleo ivyo kila mmoja ananafasi yake

“Migogoro ya ardhi haitamalizwa na kamati peke yeo, natoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha kila mtu analaani mauaji hayo na kuweka mkakati wa kutorudia kitendo kilichotokea hivi karibuni cha mauaji”alisema Askofu Mhagachi

Akielezea historia ya mgogoro wa Kiteto alisema kwa muda mrefu wananchi hao wamekuwa wakiuana hali iliyosukuma Serikali ngazi ya Taifa kuunda kamati hiyo yenye lengo moja la kutatua suluhisho la mauaji ya rejareja nay a kila mara

Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Felistas joseph ambaye ni katibu wa kamati hiyo na ni mkurugenzi msaidizi katiba na sheria na mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya kuzuia mauaji ya Kimbari na wengine ni Shekh wa Mkoa wa Arusha

Akieleza malengo ya kuundwa kamati hiyo ya Waziri Pinda mwenyekiti huyo alitaja kuwa ni pamoja na kusuluhisha wakulima na wafugaji,kupende
keza mkakati wa kudumu wa kutatua migogoro,kurejesha uadilifu na uelewa wa makundi tofauti

Malengo mengine ni kutambua kiini  cha migogoro,kuelewa mipaka ya wilaya,kutambua mpango wa matumizi bora ya ardhi toka mwaka 1961(kilima,mifugo,makazi na maeneo tengefu) na kuyaheshimu kuepuka mwingiliano ambao unaweza kuleta madhara

Kutambua makabila asili toka mwaka 1961 kuwa waliishi vipi bila migogoro na kwa sasa kilichosababisha na ufumbuzi wake ili kuepuka mauaji yasito na ulazima tena kwa watu kuuana wakifanya shuhuli zao za maendeleo wakiwa kazini

Hata hivyo ilielezwa kuwa kamati hiyo yenye uwakilishi wa  Kitaifa ina wajumbe zaidi ya kumi wamelenga kuwa endapo watafanikiwa kuutatua mgogoro huo wa ardhi itatumika katika maeneo mengine kwa mfumo uliotumika Kiteto kama eneo la majaribio

Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wakizungumza  kuhusu ujio wa kamati hiyo iliyowasili walimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kusikiliza kilio chao ambacho watu waliweza kupoteza maisha kwa kuuawa na wenzao bila sababu za msingi wakiwa kwenye makazi yao

“Nina imani kubwa na kamati hii ya maridhiano kwani wako tayari kuongea na mtu yoyote juu ya mgogoro huo, lakini pia wanapokea hata (doc) nyaraka za kuwarahisishia kazi zao”alisema Bakari Maunganya (mkulima) wa Kimana

Serikali inatumia mamilioni ya fedha kwaajili ya kuwawezesha wataalamu hao,na kwamba wananchi wawe tayari kupokea mabadiliko na kuacha kuishi maisha ya mazoea ambayo yamesababisha madhara makubwa kwa wananchi

Mwisho

Maoni