Mdiwani wa Kiteto wakiwa katika kikao cha Bajeti 2015/2016 hivi karibuni Picha na Mohamed Hamad Manyara

Madiwani vihiyo chanzo ya migogoro Kiteto

Na. Mohamed Hamad Manyara
Imeelezwa kuwa elimu ndogo kwa baadhi ya madiwani wilayani Kiteto mkoani Manyara,ushabiki wa kisiasa na ukabila ni miongoni mwa sababu zinazichangia migogoro ya ardhi wilayani humo

Hayo yameelezwa na mmoja wa wanatume tatu zilizoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye hakutaka kutajwa majina yake kwa madai kuwa sio msemaji alisema iko haja ya wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo kielimu na weledi katika kazi hizo

“Tatizo lililopo Kiteto ni ushabiki wa kisiasa,ukabila pamoja na baadhi ya wawakilishi wa wananchi (madiwani) kushindwa kutimiza wajibu wao kwa misingi ya ukabika na kuleta siasa ndani ya masuala ya kitaalamu wanapokuwa katika ngazi za maamuzi”kilisema chanzo hicho

Serikali inatumia mamilioni ya fedha kuwagharamia walaalamu zaidi ya hamsini ambao wanafanya kazi mbalimbali Kiteto zikiwemo upimaji wa ardhi, kurejesha amani kwa kufanya suluhu matokeo yao viongozi hao wamekuwa wakipingana na wataalamu hao

Awali akichangia kwenye kikao cha baraza la madiwani Sekemi Sakana Diwani wa kata ya Partimbo na Lairumbe Mollel Makamu mwenyekiti wa Halmashauri walisema kazi zinazofanywa na tume hiyo ni kuongeza migogoro na sio kutatua migogoro

“Tume inafanya kazi ya kuwapimia wakulima mashamba na kuwamilikisha huku wafugaji wakiendelea kubanwa kwa kukosa maeneo ya malisho kwani hii ndio kazi iliyowaleta kweli?alihoji Lairumbe Mollel makamu mwenyekiti wa halamshauri na Diwani Sekemi Ole Sakana wa Partimbo

Kwa upande wa Lairumbe Molleni Makamu mwenyekiti wa Halamshauri alisema tume imepata wapi mamlaka ya kugawa ardhi wakati hawapaswi kufanya hivyo, tulitegemea hawa wenzetu watusaidie sio kuongeza migogoro kama ilivyo sasa

Taarifa za uhakika zinasema akinamama wa jamii ya kifugaji (wamasai) wameandalia kupelekwa kulalamikiatatizo hilo katika maeneo mbalimbali ya Serikali Dar es Salaam na Dodoma kwa lengo la kueleza ukubwa wa tatizo hilo ili mamlaka hizo zichukuwe hatua”

Wapo akinamama wa kimasai walioenda Dar es Salaam chini ya baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali ya jamii ya kifugaji kwa lengo la kulalamikia tatizo hilo naamini watasikilizwa kwasababu kwanza ni akinamama na wao ndio waathirika wakubwa kilisema chanzo kimoja

Hata hivyo Jambo leo liliendelea kuwasaka wanatume na kupata fursa ya kuongea nao ambaye hakutaka kutajwa majina yake na kusema kuwa malalamiko ya madiwani hao ni ya kisiasa zaidi kwani wana ukabila ambao wanaendeleza ambao hauvumiliki

Alisema malalamiko ya makamu mwenyekiti wa Halmashauri limetokana na vijiji vitatu kikiwemo chake kwenda wilaya ya Kongwa baada ya kuwekwa upya mipaka kuondoa mgogoro jambo ambalo amejikuta wapiga kura wake wanakuwa upande wa pili Kongwa
“Vijiji vitatu vya Osteti,Nchinila na Engusero Engine vilivyokuwa Kiteto sasa vitasomeka Kongwa kutokana na mpaka mpya, diwani huyo analalamika kwa sababu anajua amepunguziwa wapiga kura wake sasa tunahitaji kura ama kutatua migogoro Kiteto”alihoji mtaalamu huyo na kuongeza kwa watu wapana watajua ukweli

“Kama Kiteto walishindwa na migogoro hii awali na kuomba msaada ofisi ya Waziri mkuu watulie tu watuachie tuwasaidie na tutaendelea kuwashitaki baadhi ya viongozi ambao wataendelea kufanya zoezi hili kuwa gumu”alisisitiza mtaalamu huyo

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Partimbo Sekemi Sakana alieleza kikao cha baraza la madiwani kuwa yeye ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliotuhumiwa na kushitakiwa kufanya uchochezi kwa kufanya zoezi la kuweka mipaka kuwa gumu sasa akasemee wapi

mwisho



Maoni