Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Dr Kongora akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusu madawa ya 94 mil kutakiwa kuteketezwa Picha na Mohamed Hamad Manyara
Madawa
ya 94 mil kuteketezwa Kiteto
Na.Mohamed Hamad Manyara
Imeelezwa kuwa aina mbalimbali za madawa baridi ya
binadamu ya thamani ya 94 mil katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani
Manyara yanakusudiwa kuteketezwa baada ya kubainika kuwa yamekwisha muda wake
(expired date)
Hayo yameelezwa na Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya
wilaya ya Kiteto Dr. Marting Kongora akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake waliotaka kujua changamoto zinazoikabili sekta ya Afya wilayani humo
“Tuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa aina ya dawa
ambazo zinachangiwa na bohari kuu MSD kuwa hawaleti dawa kwa wakati na
wanapoleta wakati mwingine wanayaleta yakiwa muda wake umebaki mchache”
Alisema kuwa madawa mbalimbali ya thamani ya 94 mil ya
kuanzia mwaka 1990 yakiwemo ya kurefusha maisha ARVs,TB na ya Maleria
yanatakiwa kuteketezwa baada ya kwisha muda wake
“Tunachofanya hapa Hospitali ni kupitia katika Zahanati
zote na vituo vya Afya kukagua madawa na tunapobaini kuwepo tunayakusanya na
kuyahifadhi mpaka tupate kibali ama ruhusa ya kuyateketeza”alisema Dr.Kongora
Hata hivyo changamoto ya kuteketeza madawa hayo
imejitokeza baada ya kukosemana fedha za uteketezaji pamoja na kutoandaliwa
eneo maalumu kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa wananchi
Kwa upande wa wananchi waliozungumzia kuhusu zoezi hilo
walishangazwa kusikia kuteketezwa kwa madawa hayo wakidai wakati wote waliambia
kunaupungufu wa dawa Hospitalini
“Inakuwaje dawa hizo zinateketezwa wakati kila ukifika Hospitali
ama Zahanati unaambiwa nenda kanunue dawa maduka ya watu binafsi hizi
zilizoharibika zilikuwa wapi na kwanini hazikutolewa wakati wa
kuhitajika?alihoji Joseph Kaaya (mwananchi)
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni