CELG na mkakati wa kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria Kiteto Picha na Mohamed Hamad Manyara
Wasaidizi
25 wa kisheria kiteto wajengewa uwezo
Na Mohamed Hamad Manyara
Jumla ya wasaidizi wa kisheria 25 kutoka katika kata
mbalimbali wilayani Kiteto Mkoani Manyara wameanza kupatiwa mafunzo ya siku
tano kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao
Awali akifungua mafunzo hayo Joseph Mwanga akimwakilisha Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto alisema mafunzo hayo ni mwafaka
wakati huu kutokana na kuwepo changamoto za za ukatili wa kijinsia na migogoro
ya ardhi
“Kiteto inatambulika sana hapa nchini kwa migogoro ya
ardhi kati ya wakulima na wafugaji na kwamba mafunzo haya yatakuwa mwarubaini
wa tatizo hilo”alisema Mwanga
Kwa upande wake mwezeshaji Mjengi Lissu wakili wa Kituo
cha sheria za mazingira na utawala bora (CELG) ambacho makao yake makuu yapo
Mbezi Beach Dar es Salaam alisema baada
ya washiriki kumaliza mafunzo hayo watafanya kazi kwa kipindi cha miaka miwili
wilayani humo
Alisema CELG inafanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania
bara katika Nyanja za elimu kwa jamii kuhusu sheria mbalimbali za
mazingira,maliasili na haki za binadamu
Pia kutoa msaada wa kisheria kwa jamii pamoja na usuluhishi
wa migogoro inayohusu masuala ya mazingira,ardhi na maliasili
Hata hivyo alisema kuwa Kituo kinaendelea kutoa msaada wa
kisheria kwa jamii katika wilaya ya Mafia Rufiji na Bwagamoyo chini ya ufadhili
wa Legal Service Facility
Pia kinatoa elimu ya kisheria ya utatuzi wa migogoro ya ardhi na matumizi endelevu ya ardhi katika
wilaya ya Rufiji chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society
Kuwezesha jamii juu ya utunzaji wa rasilimali za misitu
na ufugaji bora wa nyuki katika misitu ya Zumbi,Kikale,na Ngumburuni wilaya ya
Rufiji chini ya ufadhili wa mfuko wa Taifa wa Msitu (TFF)
Ambapo sasa kituo kinatekeleza na mradi wa kulinda
wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Hanang na kiteto mkoani
Manyara chini ya ufadhili wa LSF kwa
muda wa miezi 30 kwa lengo la kupunguza ukatili dhidi ya wanawake
Alisema kuwa pamoja na mambo mengine Kituo kinalenga kuwa
ifikapo 2016 huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia,kuongeza uwajibikaji
katika jamii na kuwezesha wanawake kulinda na kutetea haki zao kitafanikiwa
Kwa upande wa Mashaka Fundi,Mwadawa Ally,Musa Chambali na
Janne Isangya washiriki katika mafunzo hayo walisema ukatili wa kijinsia
wilayani Kiteto umekithiri na kwamba mafunzo hayo ni mwafaka kwa sasa
Walisema kesi nyingi zimeongezeka mahakamani katika
ubakaji,kulawiti,ambapo wamedai pamoja na jitihada hizo jamii imetakiwa kuwa
tayari kupokea elimu kutoka kwa wasaidizi hao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni