Jimbo la Kiteto lawaniwa na watano.


Jimbo la Kiteto lawaniwa na watano.

Na Mohamed hamad Manyara.
JUMLA ya watu watano wametajwa kuwania Jimbo la Kiteto lililopo mkoani Manyara kumrithi Mbunge Benedict Ole Nangoro (CCM) anayemaliza muda wake mwaka huu

Waliotajwa kuingia katika kinyanganyiro hicho ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian,Amina Saidi Mrisho (CCM) anayefanya kazi tume ya Takwimu Taifa,Jonathani Kilani kutoka CHADEMA na Mashaka Said Fundi wa SAU

Hata hivyo wakati wananchi hao wakijitokeza kuwania Jimbo hilo taarifa za uhakika kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Benedict Ole Nangoro zinaeleza kuwa anakusudia kutetea nafasi yake hiyo

“Tunahitaji wengi wajitokeze ili tuwachuje na kumpata kiongozi bora atakayekomboa Jimbo la Kiteto ambalo kwa sasa linachangamoto nyingi zikiwemo za migogoro ya ardhi” alisema mmoja wa wananchi wilayani humo

Kwa miaka saba wananchi wa Kiteto wamekuwa kwenye kipindi kigumu cha maisha kutokana na kutumia muda mwingi kwenye migogoro ya ardhi kuliko kufanya shuhuli zinhgine za maendeleo

Akizungumza hayo Ibrahimu Msindo (mwananchi) hivi karibuni alisema miaka saba iliyopita imekuwa shubiri na historia kwa wanakiteto ambapo kila mmoja anachakusema baada ya wengi wao kufanyiwa ukatili wa aina yake

“Kuna waliouawa shambani,wengine machungajini na wengine kufungwa jela kwa madai ya kuvamia maeneo na wengine kuteketezewa mali zao kutokana na ghasia zilizoibuka wilayani humo”alisema Msindo


“Tunataka Kiongozi atakaye jibu matatizo haya kati ya hao kwani mwenye mamlaka ya kumweka kiongozi madarakani ama kutomweka ni mwananchi mwenyewe na sio vinginevyo”alisema

Hata hivyo katika hatua hiyo wananchi wamewataka waliojitokeza kuwania Jimbo hilo kujipima juu ya yaliyojitokeza kwa wananchi kuuana wengine kufilisika na hata kupata vilema vya maisha kama wanatosha katika nafazi hiyo

Toka kuzindiliwa Jimbo la Kiteto mwaka 1974 wilaya ya Kiteto imeongozwa na wabunge watano akiwemo Abdalah Kimosa,Erasto Losioki, Jumanne Surumbu ambaye aliongoza kwa miezi mitatu,Benedict Kiroiya Loosurutya na Benedict Ole Nangoro aliyopo madarakani sasa.

MWISHO

Maoni