Afisa maendeleo ya jamii Joseph Mwaleba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu ya kinyanganyiro cha ubunge Jimbo la Kiteto Picha na Mohamed Hamad
WENGINE WALIOWANIA JIMBO LA KITETO AMBAO HAWAPO PICHANI NI ALLY JUMA LUGENDO,NA HAJJAT AMINA SAID MRISHO.....
NA. Mohamed Hamad Kiteto
JUMLA ya wanachama watano wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Kiteto
mkoani Manyara wamejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya
Ubunge wa Jimbo hilo
Abeid Maila Katibu wa CCM wilayani Kiteto aliwataja waliochukua fomu
hizo kuwa ni Hajjat Amina Mrisho kamishna wa Sensa Taifa 2012,Ally
Juma Lugendo mtaalamu wa kilimo na mifugo,Benedict Ole Nangoro
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kiteto,Emmanuel Papian Mtaalamu wa kilimo
na mifugo na Joseph Mwaleba Afisa Maendeleo ya Wilaya ya Kiteto
Alisema mwaka huu hakuna mbwembwe uchukuaji wa fomu akidai wote ni
watoto wa mama mmoja baba mmoja ambao wanatakiwa kuonyesha nia na
kuomba ridha kwa wanachama na atakayechaguliwa ndio ataungwa mkono na
wenzake
Katibu Maila alieleza kuwa hatua itakayofuata baadaye ni kuanza
kampeni ambazo zitakuwa tar 20.7.2015 na kuhitimishwa na uchaguzi wa
kura za maoni utakaofanyika tar 1.8.2015 kumpata atakayepeperusha
bendera ya CCM dhini ya vyama vya upinzani
Kuhusu hali ya kisiasa katibu huyo amesema kuwa Kiteto ni shwari na
hakuna tishio ndani ya chama hicho kwani hakuna chama ambacho
kinakubalika dhidi ya CCM
Mwisho

Maoni
Chapisha Maoni