22 wafanyiwa Oparesheni ya macho
Kiteto
NA MOHAMED
HAMAD MANYARA
JUMLA ya
watu 22 wenye matatizo la macho wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamefanyiwa
operesheni za kuondoa mtoto wa jicho pamoja na mtindio wa maji kwenye macho
Operesheni
hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha macho cha kanisa la Anglikan Dayosisi ya Kiteto ADC kwa ushirikiano na madaktari
kutoka hospitali ya Mvumi iliytopo mkoani Dodoma
“Watu hawa
hawakuwa wanauwezo wa kuona, walishikwa mkono kipindi chote na hata walipofika
hapa kituoni lakini baada ya kufanyiwa operesheni wanaoona naamini wanafuraha
kubwa”alisema Sis Sarawek Mbwelwa mratibu wa macho Kiteto
Alisema
Kituo cha ADK Kiteto kimekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kuwafanyia
operesheni watu wenye matatizo ya macho kuwaondolea upofu hali iliyowafanya
wakate tamaa ya kuishi maisha ya duniani
Kwa upande
wake Elizabeth Masai mmoja wa wanajamii ya kimasai wilayani humo alisema baada
ya kupata matatizo ya macho aliishi kwa kushikwa mkono na kufanyiwa kila kitu lakini
baada ya kufanyiwa operesheni sasa anaona
Alisema
Kitengo cha macho cha ADK kimekuwa msaada mkubwa sana kwake kwani hakuwa
ananufaika na mamisha ya ulimwenguni na alikata tamaa ya kuendelea kuishi akisema
alitamani kuwa bora amekufa kwa adha alizopata akiwa haoni
Akizungumzia
matatizo ya macho wilayani humo Sis Mbwelwa alisema adha hiyo inaongezeka siku
hadi siku wilayani humo kutokana
mazingira ya maisha ya wananchi yakiwemo ya uhaba wa maji na kuwa na vumbi
kipindi kirefu kwa mwaka
Katika
kukabiliana na matatizo hayo ya macho
alitoa wito kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kupima macho mara kwa mara kisha
kuchukua hatua ya tiba ambayo ndio mwarubaini wa matatizo hayo
Baadhi ya wananchi wamepongea jitihada za ADK
kuwaondolea adha ya upofu wahanga hao wa macho wakisema awali walitumia gharama
kubwa kusaka huduma hiyo mbali ambako ni Dodoma na KCMC lakini sasa inapatikana wilayani hapo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni