Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi
za CCM Kiteto
·
Gari
la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo
·
Nyumba
yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi
Na. Mohamed
Hamad Manyara
JESHI la
polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya machozi na silaha za
moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro na
Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika
kuhakiki matokeo ya Ubunge
Awali wajumbe
hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya Engusero wasifike makao
makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi
kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo
hayo
Baada ya kamati
ya siasa ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana walianza
kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na aliyekuwa mbunge wa
Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana na wajumbe hao kutaka yahakikiwe
“Baada ya
kusikia kuna kamati ya siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika
kufika ofisi za CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo
mengi matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindi”alisema mwananchi
Rajabu Jagon
Alisema
wajumbe hao waliingia ofisini ya CCM kwa zaidi ya masa 6 huku wanachama
wakisubirinje hali iliyohofiwa kuwa huenda walilenga kubadilisha matokeo hayo
na ndipo kauli za kejeli vitisho zikaanza kutolewa na baadhi ya wajumbe hao na
kuwafanya wanachama wapandwe na jazba
Christopher Ole Sendeka mjumbe wa kamati ya Siasa mkoa wa
Manyara baada ya kutoka nje alionekana
kuibua malumbano na wanachama hao wakidai aliwakashifu hali iliyowapandisha
jazba vijana hao na kuanza kurusha mawe kutaka kumpiga hali iliyowafanya polisi
kuingilia kati kunusuru
Muda mfupi Christopher
Ngubiagoi mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliyefuatana na kamati hiyo
alitoka nje kutuliza mzuka wa wanachama hao bila mafanikio na ndipo mawe
yalipoanza kurushwa na kuvunjwa kioo cha nyuma cha gari la Ole Sendeka na ndipo
Polisi wakaanza kurusha mabomu na silaha za moto juu
Tukio hilo
lilichukua takriban dakika arobaini na tano baada ya wanachama hao kupambana
ana kwa ana na polisi ofisini hapo huku wakijaribu kuwaokoa wajumbe kwa
kuwalazimisha watoke kwenye ofisi hizo kwa kurusha mabomu na kutumia silaha za
moto
Hii ni mara
ya pili kwa mbunge anayemaliza muda wake Ole Sendeka kupata wakati mgumu baada
ya dereba wake kumwondosha katika ofisi hizo mithili ya kukwepa majambazi huku
akiendelea kushambuliwa kwa mawe hadi alipotoweka katika viwanja hivyo
Katika
sakata hilo Jambo leo limeshuhudia uharibifu uliofanywa na wanachama hao kwenye
nyumba ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Ole Nangoro ikiwa imevunjwa taa
za nje kwa kama ishara ya kutomkubali katika utawala wake
Kwa mujibu
wa Christopher Ngubiagaji mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliwaambia
wanachama hao kuwa hawakuja kubatulisha matokeo, alitumwa na Katibu wa CCM
Taifa Abdurahmani Kinana kuhakiki
matokeo hayo yaliyolalamikia na mmoja wa wagombea
Pia alisemba
mbali na hilo alikuja kuona hali ya kisiasa kwa
mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kama anaweza kupambana na mgombea kupitia umoja wa vyama UKAWA
ili kuwezesha CCM kuendelea kutawala
Kufuatia kauli
hiyo mjumbe huyo alisema “mwenye macho haambiwi tazama,hana shaka na kilichoamuliwa
na wana-CCM Kiteto na kwamba ataenda kumwambia Kinana kuwa maamuzi wa
wanakiteto yanaeleweka ili naye aweze kufanya maamuzi yake
Kauli hiyo
iliungwa mkono na katibu wa CCM Wilaya Abeid Maila aliyesema kilichotokea
Kiteto hakihusishwi na kiongozi yoyote, bali wananchi waliamua kutaka kujua
hatma yao kuwa walichokifanya ni sahihi na wala hawataki kibadiliswe
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni