Nangoro abwagwa kura za maoni Kiteto


Makada wa CCM walikokuwa wakigombea nafasi ya kuwania Jimbo la Kiteto Picha na Mohamed Hamad Manyara

Nangoro abwagwa kura za maoni Kiteto
·                  Mdogo wake anusurika kuuawa ofisi ya CCM

NA. MOHAMED HAMAD KITETO
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro ameshindwa kutetea nafasi yake, na kuchukuliwa na  mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papiani kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu

Nafasi hiyo iliwaniwa na makada watano wa chama cha mapinduzi CCM akiwemo Mbunge aliyemaliza muda wake Benedict Ole Nangoro ambapo alipata kura 30,994,Emmanue Papian Mjumbe wa Halamshauri Kuu ya CCM Taifa kura 39,613

Wengine ni Hajjat Amina Said Mrisho ambaye ni kamishna wa sense nchini kura 2028,Ally Juma Lugendo mtaalamu wa kilimo na mifugo kura 330,na Joseph Mwaleba Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Kiteto 274

Kwa mujibu wa Abeid Maila katibu wa CCM wilaya akitangaza matokeo hayo jana usiku alisema kuchelewa kwa matokeo hayo kumetokana na umbali pamoja ukubwa wa eneo la Kiteto ambako maeneo mengine hayana mawasiliano ya simu

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Kiteto Alayce Ole Nangoro amenusurika kuuawa ndani ya jengo la CCM baada kuingia na kudhaniwa kuwa alienda kubadilisha matokeo yaliyokuwa yamesubiriwa kwa muda mrefu

 “Tukiwa nje tunasubiri matokeo tukaona mdogo wake Nangoro anaingia ndani ya ofisi wakati sio kiongozi  wa chama, hapo tukajua anaenda kubadilisha maotokeo na tulipomtaka atoke alijifanya mjanja kukaidi ndipo wanachama wakamuangukia”alisema mmoja wa wanachama ambaye hakutaka kutaja majina yake

Kwa upande wake Emmanue Papian Mshindi katika kura hizo za maoni aliwashukuru wanachama hao kumteua akisema huo ni mwazo wa safari na kuwaomba wananchi kumthibitisha uchaguzi mkuu ili aweze kuwatumikia

Baadhi ya wanachama wa CCM walizungumzia matokea hayo kuwa ni ,pango maalum uliokuwa wamepanga lakini pia Mungu naye aliuthibitisha kwani walifanya maombi kila kona kutaka Aliyeekuwa Mbunge huyo asiweze kupata kura za kumrudisha madarakan

“Tulifanya maombi sana kwa mungu Kiteto ni kama hatukuwa na mwakilishi, watu tulipata matatizo na hatukuwa na wakutusemea hali hii ilitugharimu na kuona njia pekee ni kurudi kwa mungu ili naye atusaidie”alisema Rajabu Jagon

Mwisho

Maoni