Wimbi la vyama vya upinzani kushinda ubunge jijini Dar es Salaam limeendelea baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika jimbo la Kinondoni, akimshinda mgombea wa CCM, Idd Azzan.
Akitangaza
matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi katika jimbo
hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty
amesema, Mtulia amepata kura 70, 337 huku Azzan aliyekuwa anatetea kiti
chake akipata 65,964.
Kwa
matokeo hayo, Kinondoni linakuwa jimbo la pili kunyakuliwa na chama
hicho katika matokeo rasmi ambayo yamekwishatangazwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) baada ya kulitwaa jimbo la Temeke lililokuwa
linashikiliwa na mwanasiasa mkongwe, Abbas Mtemvu mapema jana.
Ushindi
wa chama hicho, unafuatia ule ulioandikishwa na Chadema kwa kunyakua
majimbo ya Kawe, Ubungo, Kibamba na Ukonga, hali inayoashiria kuimarika
kwa nguvu za vyama vya upinzani jijini Dar es Salaam hasa vilivyo chini
ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kwa
mujibu wa Nec, CCM imeibuka vinara katika majimbo ya Ilala, Kigamboni
na Segerea huku matokeo ya jimbo jipya la Mbagala yakiwa hayajatangazwa.
Hadi
jana, Nec imeshatangaza matokeo katika majimbo 194 ambapo CCM imeshinda
viti vya ubunge katika majimbo 135, Chadema majimbo 34, CUF majimbo 23,
NCCR-Mageuzi jimbo moja na ACT-Wazalendo jimbo moja.
Hadi
Nec inaahirisha utangazaji wa matokeo jana, mgombea urais wa CCM, Dk.
John Magufuli alikuwa anaongoza kwa kura 2, 461, 771 sawa na asilimia
57.21 huku mgombea wa Chadema, Edward Lowassa akifuatia kwa kupata kura
1, 764, 785 sawa na 41.01.
Maoni
Chapisha Maoni