Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tar 7.Oct 1950

Mh.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizaliwa tarehe 7 Oktoba, 1950 kijiji cha Msoga kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani iliyokuwa inaitwa Tanganyika.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Msoga kati ya mwaka 1958 na 1961.
Baada ya hapo alihamia shule ya kati(middle school) Lugoba kati ya mwaka 1962 mpaka 1965. Baada ya hapo akajiunga na shule ya sekondari Kibaha kwa ajili ya O’level.

Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1966 mpaka 1969. Baada ya hapo akaelekea shule ya sekondari Tanga kwa ajili ya A’Level. Mwaka 1972 mpaka 1975 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam akisomea Uchumi.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222 248/0787 055080
Email . masarade1995@gmail.com ,
ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE

Maoni