MWILI WA DR KIGODA KUWASILI KESHO NCHINI
Marehemu Dk Abdalala Kigoda enzi za uhai wake
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdalala Kigoda
aliyefariki juzi nchini India unatarajia kuwasili tayari
kwa ajili ya mazishi.
Ofisa
habari wa Bunge, Prosper Minja ameiambia Mwananchi kuwa mwili huo
utawasili saa nane mchana kwa ndege ya Emirates na kwenda kuhifadhiwa
kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo.
Minja
amefafanua kuwa shughuli za kuaga mwili huo zitafanyika kwenye Ukumbi
wa Karimjee kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wananchi,wabunge na
viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.
“Taratibu
zote za kuaga zitafanyika Karimjee na hapo ndipo tunategemea watu wa
kada mbalimbali watafika kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk
Kigoda”amesema Minja
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi
ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa mazishi kufanyika siku ya Alhamisi.
“Kuna
kamati maalum inayohusika na msiba nadhani ikifikia uamuzi itatoa
taarifa ila ninachofahamu mazishi yatafanyika Alhamisi nyumbani kwako
Handeni” amesema Uledi
KWA MAWASILIANO PIGA 0787 055080
Maoni
Chapisha Maoni