Christian Bella na Ali Kiba
MUSA MATEJA
MKALI wa dansi mwenye asili ya Kongo,
Christian Bella amefunguka kuwa anajivunia mafanikio makubwa
waliyoyapata baada ya kufanikiwa kuingia studio na mkali wa Bongo Fleva,
Ali Kiba kuzalisha wimbo mkali ambao umeleta ladha ya Dansi na Bongo
Fleva, BongoDansi.
Akizungumza na gazeti hili, meneja wa
Bella aliyejitambulisha kwa jina la Simple, alisema Bella na Kiba
wamefanya ngoma hiyo kubwa kwenye Studio za Chedaz Record zilizopo
Mikocheni jijini Dar chini ya prodyuza Abidady ukiwa ni utunzi wa
Christian Bella.
Alisema wimbo huo ambao una ladha kali
kutoka kwa wasanii hao wakali wa Dansi na Bongo Fleva, tayari
umeshakamilika na wameshaufanyia video ambayo wameifanyia jijini Nairobi
Kenya kwa Director Enock. “Lengo ni kuleta kitu cha tofauti kwa
mashabiki.
Wimbo unakwenda kwa jina la Nagha-limia,
tayari umeshaingia kwenye vituo mbalimbali vya redio, utambulisho wa
audio ataufanya Ali Kiba kwani Bella yuko kwao Kongo kwenye matatizo ya
kifamilia. Anatarajia kurejea siku chache zijazo na akifika tu atafanya
kazi ya kuachia
Maoni
Chapisha Maoni