EU,UN WATIA SAIN KUISAIDIA TANZANIA


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) wakisaini hati ya mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000 kwa ajili ya Maendeleo Zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania. (Picha Geofrey Adroph wa 
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ruzuku kwa ajili ya Shughuli za mendeleo hapa nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakirekodi tukio hilo.
Pichani juu na chini baadhi ya wanahabari, wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya pamoja na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (katikati) baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Picha ya pamoja na mabango yenye malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

 JUMUIYA ya Ulaya (EU) imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa
Mataifa yaliyopo nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja
(One UN),ikiwa ni ruzuku ya Euro 200,000 sawa na sh. Milioni
478,000,000 fedha taslimu za kitanzania kwa ajili ya kushirikiana
katika shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazonufaisha wananchi wa
Tanzania.

Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini,
Alvaro Rodriguez na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Filiberto
Sebregondi ulifanyika katika Ofisi za EU jijini Dar es salaam na
kushuhudiwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya
Ulaya.

 Akizungumza wakati wa kutiliana saini Balozi wa Jumuiya ya Ulaya
(EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani alisema Tanzania imefanikiwa
kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza
kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.

Aidha alisema ruzuku hii imetolewa kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
imelenga kusaidia miradi ya pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU)
pamoja na Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania imekuwa ikitoa
ushirikiano katika program kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa
kama vile IOM, UNICEF, UNDP, UNODC, UNHCR, FAO, UNESCO, IFAD, UN Women
na WFP.

Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro
Rodriguez akizungumza wakati wa kutiliana saini alisema fedha hizo
zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU na UN ya mawasiliano,
uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi. Rodriguez, alisema
msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati
nchi inajipanga kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambapo
amesema

 “Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na
washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na
mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,”
 

Maoni