Gari likiwaka moto baada ya utekelezwaji wa shambulio hilo.
Utawala nchini Somalia unasema kuwa takriban watu 15wameuawa wakati wanamgambo waliposhambulia hoteli moja mjini Mogadishu.
Muonekano wa Hoteli hiyo baada ya shambulizi.
Hoteli hiyo ambayo iko kwenye moja ya mitaa yenye shughuli nyingi
mjini humo mara nyingi hutumiwa na wabunge na maafisa wa serikali, Kundi
la kiislamu la al Shabaab limekili kutekeleza shambulio hilo.Vikosi vya muungano wa Afrika vinasema kuwa vimechukua udhibiti wa hoteli hiyo baada ya mapigano. Ripoti zinasema kuwa mlipuko huo ulifuatiwa na ufyatulianaji mkubwa wa risasi.
Maoni
Chapisha Maoni