Cecafa
Hatua ya makundi ya
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge inahitimishwa leo kwa michezo miwili.
Tanzania Bara
'Kilimanjaro Stars' itamenyana na wenyeji, Ethiopia mjini Awassa katika
mchezo wa Kundi A na Uganda itapambana na Burundi katika mchezo wa Kundi
B.Kili Stars hadi sasa imejihakikishia hatua ya robo Fainali baada ya ushindi mfululizo katika mechi mbili za awali, 4-0 dhidi ya Somalia na 2-1 dhidi ya Rwanda na leo inakamilisha mechi zake za Kundi A ikiwa kileleni.
Maoni
Chapisha Maoni