Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wabunge viti maalum hadharani: CCM-64, CHADEMA-36, CUF-10



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza idadi ya wabunge wa viti maalumu ambao vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vimepata baada ya kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge nchi nzima.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema chama cha CCM ambacho kilipata jumla ya kura milioni 8.3 kimepata wabunge 64 wakati chama cha CHADEMA ambacho kilipata kura milioni 4.7 kimepata wabunge 36

CUF iliyopata kura milioni 1.2 kimepata wabunge 10, na kuainisha kuwa jumla ya wabunge wa viti maalumu vya ubunge ni viti 113 wakati viti vitano vitatoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Katika uchaguzi wa mwaka 2010, jumla ya idadi ya wabunge viti maalum ilikuwa ni 102, kwahiyo kuna ongezeko la viti 11.

Lubuva amesema orodha ya wabunge hao itawekwa hadharani na vyama husika

Maoni