Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo enzi za uhai wake.
Jeshi la Polisi mkoani Geita
linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani humo,
Alphonce Mawazo.
Kifo cha marehemu Mawazo kimetokea jana
Jumamosi Novemba 14 majira ya saa sita mchana baada ya kuvamiwa na kundi
la watu na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi.
Alphonce Mawazo akiwa na Godbless Lema.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo
amesema chanzo cha tukio hilo ni kwamba kulikuwa na mkutano wa ndani ya
Chadema uliofanyika ukumbi wa Ludete B uliokuwa unahusu mambo yao ya
uchaguzi na walipokuwa wanaendelea na kikao chao kuna mtu ambaye
anadaiwa ni mfuasi wa Chadema alikuja na na kumnong’oneza marehemu
Mawazo na baada ya hapo wajumbe walipata mshutuko na kutoka nje na
wakakutana na kundi la watu na mtafaruku ulianzia hapo.
Ameongeza kuwa tatizo hilo kutokea
kunahusishwa pia na itikadi za kisiasa lakini bado Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi wake.
Hata hivyo Kamanda Mponjoli amesema hali ni nzuri maeneo ya Katoro hasa Kata ya Ludete ambapo uchaguzi wa diwani umefanyika leo.
Maoni
Chapisha Maoni