Abraham Lincoln.
ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865
jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes.
Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.
Muhammar Muhamad Abu Migar al Ghaddaf.
MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf; alikuwa Rais wa Libya kwa miaka
42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini
Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011.
John Francis Kennedy ‘JFK’.
JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka
1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la
wazi barabarani.
Indira Priyadarshini Gandhi
INDIRA Priyadarshini Gandhi; alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984
kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini
New Delh, India.
Laurent Desire Kabila
LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa
risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.
Thomas Isdor Noel Sankara
THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi
kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi na Blaise Compaore
ambaye hivi karibuni ameikimbia nchi hiyo.
WILLIAM Richard Tolbert Jr; alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi
ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti
ndiye aliyetajwa kumuua.
Abeid Amani Karume
ABEID Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka
1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu
ambaye hakuwahi kupatikana.
NA
Jean baptist ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu,
1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua
madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.
Maoni
Chapisha Maoni