Mil 10 zarejeshwa TASAF kwa walengwa kutojitokeza





 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera akizungumza na mnufaika wa TASAF Kijiji cha Kiperesa wilayani Kiteto

Na.Mohamed Hamad Kiteto
Mil 10,428,000.00 kati ya zimetengwa na Serikali kwaajili ya kaya maskini kupitia mradi wa jamii TASAF Wilayani Kiteto mkoani Manyara zimerejeshwa makao makuu ya TASAF kutokana na walengwa 300 kutojitokeza kuchukua fedha hizo

Akizoma risala Mratibu wa TASAF wilaya ya Kiteto Phillipo.. mbelea ya mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera alisema TASAF imetoa fedha awamu mbili  kwa kaya maskini

Alisema jumla ya tsh 218,940,000.00 zilitumika katika kulipa walengwa 5,684 kwa awamu mbili Julai/Agosti, kati ya tsh 229,368,000.00 zilizoidhinishwa huku tsh 10,428,000.00 zikirejeshwa kutokana na walengwa kutojitokeza

“Mhe. Mkuu wa mkoa TASAF wilaya ya Kiteto kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Taifa kwa pamoja tuliweza kubaini kaya maskini na kuzitolea taarifa makao makuu, lakini baadhi ya wenzetu walengwa hawakujitokeza kupokea mgao huo”alisema Mratibu huyo

Mbali na changamoto hiyo kuna majina 15 hayakujitokeza kwenye malipo  jambo ambalo limesababisha manung’uniko  kwa wananchi waliokuwa wamejulishwa kusaidiwa na TASAF , alisema Mratibu huyo

Akizungumza na wananchi hao Mkuu huyo wa Mkoa Dr Joel Bender aliwatoa wasiwasi wananchi hao kuwa Serikali haitawatupa na kuwataka waandae taarifa zao vizuri na kuwasilishwa makao makuu TASAF

“Kwa wale ambao majina yao hayajaonekana hapa kuna watu 300 hawajajitokeza wasilianeni na TASAF makao makuu ambao wako tayari hapa ingizeni majina yao ili waweze kupata ruzuku hiyo”alisema Dr Bendera

Wakipaza sauti zao mbele ya mkuu huyo wa Mkoa baadhi ya wananchi wa Kijiji cah Kipereza kata ya Olboloti  akiwemo Yusuph Madi walisema msaada huo umekuja wakati mwafaka kutokana na ukwasi wa fedha walionao wananchi katika eneo hilo

Alisema katika eneo hilo wengi wao wameamua kukimbia familia zao na kwenda katika wilaya na mikoa ya jirani kutafuta maisha, huku akinamama na watoto wakiachwa wakiwa hawana kipato chochote cha kuwasaidia

“Mkuu wa Mkoa hapa tulipo kuna wezetu wamezikimbia familia zao kutokana na maisha kuwa maguni, kwa hiyo tunaiomba Serikali ione namna ya kuzito kuongeza idadi ya watu wa kuwasaidia kwani wengi wameachwa abao ni walengwa haswa” alisema

Mwisho.


Maoni