OMBI LA WABUNGE NA MADIWANI WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI KUIOMBA IKULU (OFISI YA RAIS) IUNDE TUME HURU



LEO MADIWANI NA WABUNGE WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI
tumeiomba Ikulu (OFISI YA RAIS) iteue TUME HURU YA UCHUNGUZI "a free and independent inquirery Commission" dhidi ya tuhuma za mkurugenzi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zake 3:-

 

(i) Uduni wa ubora wa barabara zilizo jengwa manispaa yabkinondoni na kushindwa kuwaadhibu wahandisi wahusika

(ii) Kushindwa kusimamia idara ya ardhi na mipangomiji ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi,


(iii) Kukosa uadilifu katika ubinafsishwaji wa fukwe za cocobeach

UKAWA MANISPAA YA KINONDONI,
tumegundua kuhusishwa na siasa za baada ya uchaguzi,kwa kuwakomoa,kufitinisha na kuadhibu wakurugenzi walioshindwa kuzuia UKAWA tusitangazwe kwenye uchaguzi mkuu 2015,sasa kwakubambikiwa tuhuma na kuhusishwa na ufisadi au uzembe......pia tumekiri ambapo tume itagundua mkurugenzi alikuwa na hatia ya ufisadi au uzembe pia awajibishwe kulingana na alichokitenda kwakuwa si dhumuni letu kutetea ubadhirifu au ufisadi

Tumekataa TAMISEMI kuhusika na hatua zinazofuata kwa uchunguzi kwakuwa wanajua kila kitu kinachoendelea katika UFISADI wa fukwe za COCOBEACH,kwakuwa ukweli wanaujua ila wameuficha na kumzunguka mheshimiwa Rais na kubambikia wengine.

TUMEUWEKA HADHARANI MAKATABA WA COCOBEACH,wananchi waone waliobinafsisha fukwe yaCOCOBEACH 2007, NA Majina ya waliotia saini mkataba huo mwaka 2007,wakati mkurugenzi Eng MUSSA NATTY,Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa KINONDONI 2013.

Ukweli huu wa kusingiziwa swala la cocobeach uwe chachu ya Tume kutafuta ukweli halisi wa tuhuma zingine,kwa kuwa TAMISEMI walihusika kila hatua ya uuzaji wa fukwe hizo.
 
chanzo CHADEMA BLOG

Maoni