Yah.Utata kuhusu vifo vya mapacha Kiteto



                                                              Mohamed Hamad  0787 055 080
Nimeamua kuandika makala hii ili juu ya utata uliojitokeza kwa wananchi wa Kata ya Bwagamoyo Kiteto.

Nini kilitokea
Jana wananchi wa Jangwani waliandamana kuhusiana na vifo vya watoto wawili mapacha ambao walitokana na operesheni, jambo hili lilileta gumzo kubwa kwa wananchi ambapo awali walisema watoto hao waliuawa na Madaktari waliomfanyia mama yao upasuaji

Katika kutaka kujua ukweli wa jambo hili nimelaimika kufanya mahojiano na DMO Kiteto ndugu wa karibu wa marehemu hao pamoja na jamaa waliokuwa katika maandamano hayo

DMO \
Swali..Dr naitwa Mohamed Hamad nimekuja kutaka ufafanuzi juu ya vifo vya watoto wawili mapacha waliofariki kutokana na operesheni ya juzi usiku na kusababisha jana watu kuandamana kuwa mmoja wao ametenganishwa kichwa na kiwiliwili hilo likoje Dr...

Jibu..Ni kweli kulikuwa na mama mmoja mwenye umri wa miaka 18 aliletwa kutoka kata ya Bwagamoyo akiwa mja mzito na baada ya vipimo ilionekana kuwa alitakiwa ajifunguwe tar 11.1.2015 lakini alianza kuumwa uchungu kabla ya muda

Baada ya kuendelea kuumwa alifanikiwa kujifungua mtoto akiwa mfu alitanguliza miguu na baadaye ikaonekana kuwa na mtoto mwingine hapo ilikuwa kazi kumtoa kutokana na kukatisha tumboni

Baada ya jitihada kubwa aliweza kupata mwelekeo lakini naye alitanguliza miguu kama yule wa mwanzo ambapo hapo baada ya jitihada alijaribu kutanguliza miguu na kuanza kutolewa lakini ilishindikana na kufanyiwa upasuaji

Katika Jitihada hizo kwakuwa mtoto huyo naye alikuwa mfu baada ya vipimo ilibidi zitumike jitihada za kumwokoa mama yao ambapo kiutaalamu mtoto akifia tumboni kabla ya upasuaji unaweza kutumia jitihada zozote kumwokoa mama yake kama ilivyotokea

....kutokana na jitihada hizo Dr huyo ambaye alikuwa na cheo cha juu katika hospitali hiyo aliweza kuzungumza na familia na kuelezana yaliyotokea kisha kukubaliana nao na kubeba miili hadi nyumbani

.......Kilichotokea ni familia hiyo kushawishiwa na majirani kisha kurejesha marehemu hao hospitalini tena kwa maandamano kwa madai wameuawa na Madaktari jambo ambalo lilileta usumbufu na taaruki kwa kwa baadhi ya wananchi na hata madaktari

Baadhi ya viongozi waliofika hapo ni pamoja na usalama wa taifa, Mbunge, uongozi wa Polisi na viongozi wengine waandamizi na kuunda jopo la madaktari watatu kuchunguza vifo hivyo, ambapo kwa kujibu wa daktari huyo alisema operesheni hiyo sio ya kwanza kufanyika  kwani baada ya hiyo zimeendelea kufanyika katika kuokoa wazazi waliokuwa na matatizo hayo kwa siku hiyo

Kwa mujibu wa Dr huyo alisema mama aliyokuwa anaokolewa maisha yake afya inaimarika anaendelea na matibabu huku familia ikiwa imeshauriwa kwenda kuzika marehemu hao

NDUGU
Baadhi ya ndugu waliozungumzia tukio walikiri kumpeleka ndugu yao wakisema alikuwa mjamzito na alienda kufanyiwa upasuaji na kutolewa watoto wawili wafu baadaye walizungumza na madaktari yaliyotokea na kukubaliana nao kwenda kuzika

Wakiwa huko walipata ushauri na kuonekana watoto hao wameuawa kisha kuwarejesha hospitali ambapo baada ya ufafanuzi wa kina tena waliwachukuwa na kwenda kuwazika katika makaburi ya Jangwan Kiteto​

Mbunge E Emmily Papian​
Suala hili limeshuhulikiwa kisheria na ndugu tumeshauriana wachukue miili na kwenda kuzika...

"Hii operesheni sio ya kwanza zimeendelea kufanyika na wengi wameokolewa sasa kilichotokea ni teknic tu ya kutaka kuokoa mama mzazi"alisema Mhe Mbunge huyo

NDUGU NA JAMAA
Tuliona watoto wakiwa wana majeraha tukaona sio hali ya kawaida tukasema nivyema tukapata ufafanuzi waliopata ufafanuzi wa kwanza hawakuwa na majibu ya kutosha ndio maana tukalazimika kuja tena tukiwa katika maandamani

Haya ni machache kati ya niliyoweza kuyapata kutokana na sakata la vifo vya watoto hao ambapo pamoja na kuundwa JOPO la kuchunguza wamekubaliana kwenda kuzika watoto hao hali ya mzazi aliyekuwa anaokolewa inaimarika





Naendelea kufuatilia nitawajuza jamani...

Maoni