Agizo la Rais lapuuzwa Kiteto

                                                                               Rais JPM wa tanzania

Agizo la Rais lapuuzwa Kiteto

MOHAMED HAMAD
Wakati kukiwa na agizo la Rais John Pombe Magufuli kuwa kutakuwa na
elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, agizo hilo
limepuuzwa Wilayani Kiteto kwa wazazi kushurutishwa kutozwa tsh 20,000
debe 4 za mahindi na maharagwe debe 2 kwa miezi sita wanafuni watakao
kaa shuleni

Kwa mujibu wa barua yenye KUMB.NA.LESS/F:1/2016/01 iliyoandikwa na
Parkosidi Kambi mkuu wa shule ya sekondari Lesoit tar 26/12/2016 kwa
wazazi wa wanafuzi waliofaulu kujiunga na shule hiyo imeeleza kuwa,
hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mzazi atakayeacha kumfikisha
mwanafunzi shuleni akiwa hana mahitaji yaliyo orodheshwa kwenye barua
hiyo

Katiba barua hiyo pia imeeleza kuwa shule ni ya bweni kwa wavulana na
wasichana wanatakiwa kufika wakiwa na godoro la futi mbili na nusu,
shuka za kimasai mbili, kiti kimoja na meza yake, na panga au fyekeo
vitakavyotumika hapo shuleni hapo

Akizungumza na MTANZANIA mmoja wa wazazi hao ambaye hakutaka kutaja
majina yake kuandikwa, alisema kwa maelekezo haya inaonyesha kuwa
maagizo haya yatakuwa na manufaa kwa uongozi wa shule kutokana na
wazazi kulazimishwa huku kukiwa na agizo la Serikali kugharamia
michango hiyo

“Kinachotushangaza wazazi na ambacho jibu lake hatujawahi kupata hata
siku moja ni kuhusu kushurutishwa kiti na meza kwa kila mwanafunzi
anayejiunga na sekondari, haya madawati mbona hatuoni mabaki yake hata
kama yamechakaa huwa yanaenda wapi”alihoji mzazi huyo

Alisema mara nyingi kumekuwepo na ujanja ujanja wa waalimu kuagiza
wanafunzi fedha ama vifaa na kuvitumia wao nyumbani ama kuuza wapate
fedha jambo ambalo wazazi wanageuzwa kama vyanzo vya mapato yao

Kwa upande wake Bakari Maunganya (mwananchi) alisema uongozi wa wilaya
hauwezi kukwepwa na uongozi wa wilaya ya Kiteto ambao siku zote wapo
wanaona maagizo hayo na hawachukui hatua kwa wahusika akisema iko haja
ya viongozi hao kuwa wazalendo

Kwa mujibu wa Samuel Nzoka Mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani manyara
kuhusu barua hiyo amesema, hajaiona na kusisitiza kuwa atafuatilia na
kudai Serikali haijakataza michango yote bali kuna baadhi ya michango
lazima wazazi wachangie ili kuboresha shule yao

mwisho

Maoni