Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewaambia viongozi wa Afrika
kwamba anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka
amani huko Burundi.
Alisema
hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za AU nchini Ethiopia, ambako
viongozi hao watapiga kura kuunga mkono au kukataa pendekezo hilo.
Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amelipinga pendekezo hilo - Burundi inasema kutuma wanajeshi huko itaonekana kama uvamizi.
Uamuzi wa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa uongozi ndiyo uliozusha ghasia za miezi kadha.
Kiongozi
wa Gambia, Yahya Jammeh, ambaye alinyakua madaraka kwa kupindua
serikali, alisema hatounga mkono pendekezo hilo iwapo Burundi
haitoridhia.
Na rais wa Chad, Idris Deby, amepokea nafasi ya uenyekiti wa AU kutoka kwa kiongozi wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Maoni
Chapisha Maoni