UZINDUZI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF WILAYANI KITETO MANYARA








Mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanali Samuel Nzoka akizindua mfuko wa CHF
kata ya Dosidosi na Dosodosi

DC Kiteto awataka wananchi kujiunga na CHF

NA.MOHAMED HAMAD
MKUU wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Kanali Samuel Nzoka, amewataka
wananchi wilayani humo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili
kuboresha huduma hiyo ambayo inadaiwa kudhorota

Akieleza hayo kwenye uzinduzi wa mfuko huo uliofanyika kata za
magungu, Engusero na Dosidosi wilani humo Kanali Nzoka alisema,
kuboreka kwa huduma
ya afya ya jamii katika vituo kutatokana na wananchi wengi kujiunga na
mfuko wa CHF

Alisema vituo vya afya, Zahanati na hata Hospitalini vina upungufu
mkubwa wa dawa kutokana na uchangiaji hafifu wa wananchi katika huduma
hiyo na kuwataka wananchi kujiunga na CHF ili waweze
kupata dawa za kutosha kwa mfumo wa tele kwa tele

“Rais wa awamu ya kwanza (marehemu) mwalimu nyerere alisema, umoja ni
nguvu na utengano ni udahifu, akimaanisha shilingi 10,000 haiwezi
kukidhi mahitaji ya mtu mmoja ama idadi ya watu sita lakini kwa umoja
huo fedha hizi zikichangwa kwa wingi zinatosha kuondoa tatizo”alisema

Akizungumza na wananchi hao meneja wa Bima ya afya mkoa wa manyara
Isaya Henry Shekifu alisema mpango huu uliana mwaka 2001 na unahudumia
Halmashauri 144 nchini ambazo baada ya kufanya vizuri katika michango
yao zimelipwa bil 7.9 kama madai ya tele kwa tele

Alisema tiba ya mgonjwa mmoja kwa shilingi 10,000 kwa mwaka tena
wakiwa watu 6 ni maajabu kwa baadhi ya watu akisisitiza kuwa kama
itapatikana  mil 300 kwa mwaka wilayani humo hakutakuwa tatizo la
wananchi kukosa dawa wilayani Kiteto

Alidai kuwa mkoa wa manyara wakazi ni 5% tu ya wananchi wanaohudumiwa
kati ya kaya laki 320, huku wilaya ya kiteto ikishika mkia kwa kuwa na
idadi ndogo katika kuchangia mfuko huo sawa na 2% ya idadi ya wananchi
waliojiunga na mfuko huo

Kwa upande wa Saidi shambani, Binaisa Issa na Anjelina Lazaro wananchi
wa kata ya Engusero walisema mfuko ni mzuri na kuomba changamoto
zilizopo kutatuliwa kwanza kuwa wamekuwa wakikosa dawa kwenye zahanati
na vituo vya afya huku majibu yakitolewa kuwa Serikali haina fedha za
kununulia dawa

“Tunataka viongozi watuhakikishie endapo tutajiunga kwa kutoa shilingi
elfu 10,000 na dawa zikakosekana kwenye eneo husika waende wapi ili
kupata huduma hiyo kwani imekuwa ni mazoea sasa kila kituo cha afya
kwa kusema hakuna dawa wananchi wakanunue maduka ya watu binafsi”

Akijibu Swali hilo mratibu wa mfuko wa afya ja jamii Bw. Shekifu
aliwahakikishia wananchi hao kuwa michango yao itakuwa mikono salama
ikilenga kuondoa adha ya uhaba wa dawa za binadamu kwa kuwataka
wajitokeze kwa wingi wako tayari kufanikisha zoezi hulo

mwisho

Maoni