Mkurugenzi
Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana
Yassoda leo amefunga kozi ya ukocha wa wanawake ngazi ya juu (High
Level Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.
Akiongea
wakati wa kufunga kozi hiyo, Mama Yassoda amesema anaishukuru TFF/FIFA
kwa kuona wanawake wanapata nafasi ya kushiriki kozi mbalimbali, ikiwemo
kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya juu kwa wanawake.
Mama
Yassoda amewataka washiriki wa kozi hiyo kuyafanyia kazi mafunzo
waliyopatiwa katika kuhamasisha wanawake wengi kuupenda mpira wa miguu
na kuzalisha vipaji vya wachezaji wengi wa kike kuanzia ngazi za chini,
na sio kuhitimu na kuweka vyeti ndani tu.
Naye
Mariam Mchaina akiongea kwa niaba ya washiriki wenzake, ameishukuru TFF
kwa kuwakumbuka wanawake na kuwapatia kozi hiyo ya ukocha, na kuahidi
watakaporudi sehemu wanazoishi watatumia ujuzi walioupata kufundisha
wanawake mpira miguu kwa ngazi zote.
Kozi
hiyo ya ukocha kwa wanawake, ilianza Jumatatu na kumalizika leo ambapo
jumla ya washiriki 25 wameshiriki kozi hiyo ya awali kutoka katika mikoa
ya Dar es salaam, Iringa, Ruvuma, Pwani na Tanga na kupewa vyeti ya
ushiriki na mpira kama kifaa cha kuanzia kazi ya ukocha.
Maoni
Chapisha Maoni