MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA NA VIONGOZI WAKE WAFANA JIJINI DAR ES SALAAM


Friday, January 1, 2016
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, akihutubia kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa,Dua Maalum ya kuwaombea viongozi na Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Mchungaji Eden Godfrey akihubiri kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, Dua maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

 Viongozi wakiwa wameshikana mikono wakati wa maombi maalum kwa Taifa na Viongozi wake .
 Umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye ibada maalum ya mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
 Wananchi wakiwa kwenye maombi ya kuliombea Taifa Amani, na kuwaombea viongozi wake afya njema.
 Mwalimu Teddy Kwilasa akitoa maombi maalum kwa Taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya.
 Wananchi wakiwa kwenye maombi mazito ya kuwaombea Viongozi wa Taifa letu
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa pili kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na wake zao wakiupokea mwaka kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, ambapo Taifa na Viongozi wake waliombewa.
 Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye mkesha mkubwa uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam maalum za kuwataka wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa amani ya nchi wakati wa mkesha wa mkubwa kitaifa wa kuombea Taifa na Viongozi wake dua maalum.
 Bi. Christina Elias wa Aleluyah kwaya kutoka Tabata  akiimba kwa hisia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wakiwa kwenye maombi maalum ambapo waliwakilisha Mawaziri wote nchini.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NAPE AZINDUA FILAMU INAYOONYESHA MASUALA YA RUSHWA

Wednesday, December 30, 2015

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa na mtangazaji mashuhuri wa Azam TV Taji Liundi muda mfupi kabla ya kuzindua filamu mpya ya Home Coming kwenye ukumbi wa Century Cinema ,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa Sanaa na Utamaduni wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa filamu mpya ya Home Coming.
 Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo ya Home Coming ,Susan Lewis maarufu kama Natasha
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Ayo TV muda mfupi kabla ya kuzindua Cinema ya Home Coming.
Muigizaji mkuu wa filamu ya Home Coming Daniel Kijo (kushoto) akisalimana na mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo kufanyika kwenye ukumbi wa Century Cinema, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI KIGOMA

Monday, December 28, 2015
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalikiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo leo Desemba 28, 2015. Kushoto ni Mwenye kiyi wa CCM wa mkoa wa Kigoma, Walid Kabourou. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Muu, Kassim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo leo Desemba 28, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya

VIDEO: DK. MAGUFULI AWAPISHA MAWAZIRI ALIOWATEUA WIKI ILIYOPITA

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAPYA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Mawaziri wapya wakisubiri kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mawaziri wapya wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni  baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa  Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua  kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) kuwa  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.   Profesa Makame Mbarawa (kulia) (amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Hamad Masauni (kulia) kuwa  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya wanne na Manaibu Waziri leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha. Wa pili kushoto mstari wa mbelel ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa.(Picha zote na Benedict Liwenga)

Maoni