Njaa Kiteto yakimbiza wanaume


MOHAMED HAMAD
Baadhi ya wananume wilayani Kiteto mkoani manayara, wamedaiwa kutoroka
familia zao kutokana na tatizo la njaa lililojitokeza hali iliyosukuma
Serikali wilayani hamo kuagiza tani 500 mahindi  kukabiliana na tatizo
hilo

Akizungumza hayo Yusuph Madi (mwananchi) wa Kijiji cha Kiperesa mbele
ya mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera hivi karibuni alisema idadi
kubwa ya wanaume kijijini hapo wametoroka familia zao na kwenda
kusikojulikana

“Mhe. Mkuu wa mkoa Serikali angalieni namna ya kutusaidia wananchi juu
ya tatizo la njaa, kuna kundi kubwa la wenezu (wanaume) wametoroka
familia zao na kuacha wanawake na watoto kutokana na tatizo la
njaa”alisema

Kama hakutakuwa na jitihada za maksudi madhara makubwa yatajitokeza
yakiwemo vifo vya watu kutokana na kukosa chakula kwani chakula ndio
kila kitu hapa alisisitiza madi wakati akieleza kilio hicho kwa mkuu
huyo wa mkoa

Akizungumza na wananchi Mkuu huyo wa mkoa alisema, serikali imetoa
chakula awamu ya kwanza bure na sasa tani 500 tena zimeagizwa kwaajili
ya wananchi kuuziwa na wafanya biashara kwa bei ya chini

Kwa mujibu wa Yahaya Issa (mwananchi) alisema Serikali inatakiwa
kuendelea kutoa chakula hicho bure kwa wananchi wake kutokana ukwasi
uliojitokeza kuwa hakuna fedha ya kununua chakula na ndio maana
wengine wanakimbia familia zao

Akizungumza na MTANZANIA Nicodemus John katibu tawala wa wilaya ya
Kiteto amesema chakula hicho kilipaswa kufika toka wiki moja iliyopita
kimechelewa Songea kutokana na msongamano wa magari yanayobeba chakula
hicho

mwisho

Maoni