Njaa yatisha maisha ya wanaoishi na VVU Ukimwi Kiteto

                      Picha ya maktaba... Rais Mstaafu wa Tanzania J M Kikwee akikagua ghala la chakula

Njaa yatisha maisha ya wanaoishi na VVU Ukimwi Kiteto

MOHAMED HAMAD KITETO
Zaidi ya watu 500 wanaoishi na VVU Ukimwi wilayani Kiteto mkoani
Manyara, wanahofu ya kuendelea kuishi kutokana na Serikali pamoja na
wadau mbalimbali wa maendeleo kusitisha misaada ya vyakula

Awali WAVIU hao walipata misaada ya unga wa  lishe, mafuta, pamoja na
mahindi ya kusaga, wakati wakiendelea kutumia dawa za kurefusha maisha
na baadaye kusitishwa kutokana na sababu mbalimbali kutoka kwa
wanaotoa misaada hiyo

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yake gazetini mmoja wa
wanaoishi na VVU Ukimwi wilayani Kiteto alisema taarifa wanazopata
kutoka Serikalini ni kwamba hawana fedha kwa hivi sasa hivyo watafute
namna mbadala ya kuishi

“Kila mara tunalazimika kwenda ofisi za maendeleo ya jamii Kiteto
kuulizia kama Serikali imepata fedha bila mafanikio…naiomba Serikali
ione umuhimu wa kuokoa maisha yetu ambayo kwa sasa yako hatarini
kutokana na kukosa chakula”

Akizungumza na MTANZANIA Joseph Mwaleba Afisa maendeleo ya jamii
wilaya ya Kiteto alisema, jitihada za serikali zimekoma baada ya
kukosekana fedha za kuwasaidia na badala yake wamehamasihwa kuunda
vikundi vya ujasiria mali ili fedha ikipatikana wapatiwe
Alisema mwaka jana Halmashauri ya wilaya Kiteto ilitoa kiasi cha mil
10 kwaajili ya vikundi 20 vya watu wanaoishi na VVU Ukimwi kwa lengo
la kuwajengea uwezo wa kipato cha mtu mmoja mmoja ili kuondokana na
utegemezi

“Serikali kuendelea kutoa msaada kila siku kwa watu wanaoishi na VVU
Ukimwi haina tija, tulikaa na kubuni njia ya kuwasaidia kwa kuanzisha
vikundi vya ujasiria mali ili waweze kufanya biashara za kuwaingizia
kipato”alisema Mwaleba

Kwa upande wake Kanti Greogori Marandu mwenyekiti wa kanisa la Roman
Catholic parokia ya Kibaya alisema walikuwa na utamaduni wa kutoa
misaada kwa watu waishio na VVU Ukimwi kutoka Jimbo la Arusha lakini
sasa imesitishwa

“Tulikuwa na kitengo cha kuwasaidia chakula kama vile unga wa lishe kg
50 mahindi debe 4 maharagwe pamoja na mafuta lita tano laiki sasa
kimesitishwa mpaka hapo watakapojipanga tena Jimboni”

Alisema msaada huo ulikuwa unatolewa na WFP na kukabidhiwa viongozi wa
kanisa la RC mkoa wa Arusha kisha kutawanya kwenye parokia zake ambapo
hapo walengwa walinufaika ila sasa imesitishwa na naamini madhara ni
makubwa sana kwa kukosa misaada hiyo

Kwa mujibu wa Dk Malisa anayeshuhulikia kitengo cha Ukimwi Hospitali
ya wilaya ya hospitali amekiri kuwepo adha kubwa kwa watu waishio na
VVU Ukimwi wilayani humo akisema kusitishwa misaada ni tishio kwa watu
wanaoishi na VVU Ukimwi

“Hizi dawa zinahitaji mtu ale na ashibe na kwa wale ambao kinga zao
zimeshuka sana wanahitaji mlo mzuri ambao ni ule waliokuwa wanaupata
kutoka serekalini na mashirika yasiyo ya kiserikali ila sasa hawapati
”alisema Dr Malisa

mwisho

Maoni